Leviticus 19:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho kwa kutumia kondoo huyo mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya dhambi aliyotenda; naye atasamehewa dhambi hiyo aliyotenda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kupitia kwa huyo kondoo dume wa sadaka ya hatia, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya dhambi aliyotenda, naye atasamehewa dhambi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, kwa huyo kondoo mume wa sadaka ya hatia mbele za Bwana, kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya; naye atasamehewa hiyo dhambi yake aliyoifanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho kwa kutumia kondoo huyo mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya dhambi aliyotenda; naye atasamehewa dhambi hiyo aliyotenda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pamoja na kondoo dume wa sadaka ya hatia, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA kwa ajili ya dhambi aliyotenda, naye atasamehewa dhambi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kupitia kwa huyo kondoo dume wa sadaka ya hatia, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za bwana kwa ajili ya dhambi aliyotenda, naye atasamehewa dhambi yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, kwa huyo kondoo dume wa sadaka ya hatia mbele za BWANA, kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya; naye atasamehewa hiyo dhambi yake aliyoifanya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho kwa kutumia kondoo huyo mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya dhambi aliyotenda; naye atasamehewa dhambi hiyo aliyotenda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mtambikaji na ampatie upozi na kumtoa yule dume la kondoo kuwa ng'ombe ya tambiko ya upozi mbele ya Bwana kwa ajili ya kosa lake, alilolikosa; ndipo, atakapoondolewa hilo kosa lake, alilolikosa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha huyo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, kwa huyo kondoo mume wa sadaka ya hatia mbele za BWANA, kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya; naye atasamehewa hiyo dhambi yake aliyoifanya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani atamufanyia ibada ya upatanisho kwa kutumia kondoo huyo mbele ya Yawe kwa ajili ya zambi aliyotenda, naye atasamehewa zambi hiyo aliyotenda.