Leviticus 19:31 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Msiwaendee waaguzi wa mizimu wala wachawi ili kuwaomba wawaagulie na hivyo mkajitia najisi. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Msiende kwa waaguzi, wala msitafute wapunga pepo, kwa maana watawanajisi. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Msiwaendee waaguzi wa mizimu wala wachawi ili kuwaomba wawaagulie na hivyo mkajitia najisi. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Msiwaendee waaguzi, wala msitafute wapunga pepo, kwa maana watawanajisi. Mimi ndimi BWANA Mungu wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Msiende kwa waaguzi, wala msitafute wapunga pepo, kwa maana watawanajisi. Mimi ndimi bwana Mwenyezi Mungu wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Msiwaendee waaguzi wa mizimu wala wachawi ili kuwaomba wawaagulie na hivyo mkajitia najisi. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Msiwageukie waganga wa kutiisha mizimu wa waaguaji. Msiwatafute, mkajipatia uchafu kwao. Mimi Bwana ni Mungu wenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musiwaendee waaguzi wa mizimu wala wachawi kwa kuwaomba wawaaguzie. Mukifanya hivi, mutajichafua. Mimi ni Yawe, Mungu wenu.