Leviticus 19:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mnaponitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka za amani, mtanitolea kama itakiwavyo ili mpate kukubaliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Mnapotoa dhabihu ya sadaka ya amani kwa Mwenyezi Mungu, toeni kwa namna ambayo itakubaliwa kwa niaba yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi hapo mtakapomchinjia Bwana sadaka ya amani mtaisongeza ili kwamba mpate kukubaliwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mnaponitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka za amani, mtanitolea kama itakiwavyo ili mpate kukubaliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Mnapotoa dhabihu ya sadaka ya amani kwa BWANA, toeni kwa namna ambayo itakubaliwa kwa niaba yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Mnapotoa dhabihu ya sadaka ya amani kwa bwana, toeni kwa namna ambayo itakubaliwa kwa niaba yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi hapo mtakapomchinjia BWANA sadaka ya amani mtaitoa kwa njia ipasayo ili mpate kukubaliwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mnaponitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka za amani, mtanitolea kama itakiwavyo ili mpate kukubaliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtakapomtolea Bwana ng'ombe ya tambiko ya shukrani, sharti mwitoe hivyo, atakavyopendezwa nanyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi hapo mtakapomchinjia BWANA sadaka ya amani mtaisongeza ili kwamba mpate kukubaliwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munaponitolea mimi Yawe sadaka za amani, mutanitolea kama vile inavyotakiwa kusudi mupate kukubaliwa.