Leviticus 20:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama mwanamume yeyote akilala na mwanamume mwenzake kana kwamba ni mwanamke, basi, wote wawili ni lazima wauawe kwani wamefanya jambo lililo chukizo; watawajibika kwa umwagaji wa damu yao wenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Kama mwanaume akikutana kimwili na mwanaume mwenzake kama vile mwanaume afanyavyo na mwanamke, wanaume hao wawili wamefanya lililo chukizo sana. Lazima wauawe; nayo damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama mwanamume yeyote akilala na mwanamume mwenzake kana kwamba ni mwanamke, basi, wote wawili ni lazima wauawe kwani wamefanya jambo lililo chukizo; watawajibika kwa umwagaji wa damu yao wenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Kama mwanaume akikutana kimwili na mwanaume mwenzake kama vile mwanaume afanyavyo na mwanamke, wanaume hao wawili wamefanya lililo chukizo sana. Lazima wauawe; nayo damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Kama mwanaume akikutana kimwili na mwanaume mwenzake kama vile mwanaume afanyavyo na mwanamke, wanaume hao wawili wamefanya lililo chukizo sana. Lazima wauawe; nayo damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mwanamume akilala pamoja na mwanamume, kama alalavyo na mwanamke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama mwanamume yeyote akilala na mwanamume mwenzake kana kwamba ni mwanamke, basi, wote wawili ni lazima wauawe kwani wamefanya jambo lililo chukizo; watawajibika kwa umwagaji wa damu yao wenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu akilala na mwanamume mwingine, kama wanavyolala na mwnamke, wamefanya tapisho, wote wawili sharti wauawe, maaana wamekora manza za kumwagwa damu zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mwanaume yeyote akilala na mwanaume mwenzake sawa vile ni mwanamuke, basi, wote wawili wanapaswa kuuawa maana wamefanya jambo linalokuwa chukizo na damu yao itakuwa juu yao wenyewe.