Leviticus 20:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama mwanamume akilala na mwanamke aliye mwezini, wote wawili ni lazima watengwe na watu wao; huyo mwanamume amelala na mwanamke aliye na hedhi, na huyo mwanamke amelala na mwanamume akiwa na hedhi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Ikiwa mwanaume atakutana kimwili na mwanamke aliye katika hedhi yake, amefunua mtiririko wa hedhi yake, naye huyo mwanamke amejifunua uchi wake. Wote wawili lazima wakatiliwe mbali na watu wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mtu mume akilala na mwanamke aliye na ugonjwa wake, na kufunua utupu wake; amelifunua jito la damu yake, naye mwanamke amefunua jito la damu yake; wote wawili watakatiliwa mbali na watu wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama mwanamume akilala na mwanamke aliye mwezini, wote wawili ni lazima watengwe na watu wao; huyo mwanamume amelala na mwanamke aliye na hedhi, na huyo mwanamke amelala na mwanamume akiwa na hedhi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Ikiwa mwanaume atalala na mwanamke aliye katika hedhi yake na kukutana naye kimwili, amefunua mtiririko wa hedhi yake, naye huyo mwanamke amejifunua uchi wake. Wote wawili lazima wakatiliwe mbali na watu wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Ikiwa mwanaume atalala na mwanamke aliye katika hedhi yake na kukutana naye kimwili, amefunua mtiririko wa hedhi yake, naye huyo mwanamke amejifunua uchi wake. Wote wawili lazima wakatiliwe mbali na watu wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mwanamume akilala na mwanamke aliye na ugonjwa wake, na kufunua utupu wake; amefunua jito la damu yake, naye mwanamke amefunua jito la damu yake; wote wawili watatengwa mbali na watu wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama mwanamume akilala na mwanamke aliye mwezini, wote wawili ni lazima watengwe na watu wao; huyo mwanamume amelala na mwanamke aliye na hedhi, na huyo mwanamke amelala na mwanamume akiwa na hedhi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu akilala na mwanamke aliye miezini, akiufunua uchi wake na kukitokeza waziwazi kijito chake, naye mwanamke akikifunua kijito cha damu yake, wote wawili sharti wang'olewe katikati yao walio ukoo wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mtu mume akilala na mwanamke aliye na ugonjwa wake, na kufunua utupu wake; amelifunua jito la damu yake, naye mwanamke amefunua jito la damu yake; wote wawili watakatiliwa mbali na watu wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mwanaume akilala na mwanamuke anayekuwa na ugonjwa wa mwezi, wote wawili wanapaswa kutengwa na watu wao; huyo mwanaume amelala na mwanamuke aliyekuwa na ugonjwa wa mwezi, na huyo mwanamuke amefunua mutiririko wa damu yake.