Leviticus 20:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Usilale na dada ya mama yako wala na shangazi yako, maana hao ni jamaa yako wa karibu. Wote watendao hayo watawajibika kwa uovu wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Usikutane kimwili na dada wa mama yako wala wa baba yako, kwa maana hilo litamwaibisha jamaa wa karibu; ninyi wawili mtawajibika kwa ajili ya uovu huo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Usifunue utupu wa umbu la mama yako, wala umbu la baba yako; kwa kuwa huyo amefunua utupu wa jamaa yake ya karibu; watauchukua uovu wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Usilale na dada ya mama yako wala na shangazi yako, maana hao ni jamaa yako wa karibu. Wote watendao hayo watawajibika kwa uovu wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Usikutane kimwili na dada wa mama yako wala wa baba yako, kwa maana hilo litamwaibisha jamaa wa karibu; ninyi wawili mtawajibika kwa ajili ya uovu huo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Usikutane kimwili na dada wa mama yako wala wa baba yako, kwa maana hilo litamwaibisha jamaa wa karibu; ninyi wawili mtawajibika kwa ajili ya uovu huo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Usifunue utupu wa dada ya mama yako, wala dada ya baba yako; kwa kuwa huyo amefunua utupu wa jamaa yake ya karibu; watalipizwa kwa uovu wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Usilale na dada ya mama yako wala na shangazi yako, maana hao ni jamaa yako wa karibu. Wote watendao hayo watawajibika kwa uovu wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Uchi wa mama yako mkubwa na mdogo nao uchi wa shangazi yako usiufunue, kwani ni kuutokeza waziwazi uchi wao walio ndugu wa kuzaliwa nao; hizo manza, walizozikora, zitawakalia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Usifunue utupu wa umbu la mama yako, wala umbu la baba yako; kwa kuwa huyo amefunua utupu wa jamaa yake ya karibu; watauchukua uovu wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Usilale na dada ya mama yako wala na shangazi yako, maana hao ni jamaa yako wa karibu. Wote wanaotenda vile watabeba lazima ya uovu wao.