Leviticus 20:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Waambie Waisraeli hivi: Mtu yeyote miongoni mwa Waisraeli au mgeni anayekaa miongoni mwenu, akimtoa sadaka mtoto wake yeyote kwa mungu Moleki ni lazima mtu huyo auawe. Wananchi wa hapo watamuua kwa kumpiga mawe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Waambie Waisraeli: ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi Israeli atakayemtoa kafara mtoto wake yeyote kwa Moleki lazima auawe. Watu wa jumuiya hiyo watampiga kwa mawe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena uwaambie wana wa Israeli, Mtu awaye yote miongoni mwa wana wa Israeli, au miongoni mwa wageni waketio katika Israeli, atakayetoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, sharti atauawa; wenyeji wa nchi watampiga kwa mawe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Waambie Waisraeli hivi: Mtu yeyote miongoni mwa Waisraeli au mgeni anayekaa miongoni mwenu, akimtoa sadaka mtoto wake yeyote kwa mungu Moleki ni lazima mtu huyo auawe. Wananchi wa hapo watamuua kwa kumpiga mawe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sema na wana wa Israeli: ‘Mwisraeli ye yote au mgeni anayeishi katika Israeli ambaye atamtoa ye yote miongoni mwa watoto wake kuwa sadaka kwa mungu Moleki, mtu huyo lazima auawe. Watu wa jumuiya hiyo watampiga kwa mawe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sema na wana wa Israeli: ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi katika Israeli ambaye atamtoa yeyote miongoni mwa watoto wake kuwa sadaka kwa mungu Moleki, mtu huyo lazima auawe. Watu wa jumuiya hiyo watampiga kwa mawe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena uwaambie wana wa Israeli, Mtu yeyote miongoni mwa wana wa Israeli, au miongoni mwa wageni waishio katika Israeli, atakayetoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, sharti atauawa; wenyeji wa nchi watampiga kwa mawe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Waambie Waisraeli hivi: Mtu yeyote miongoni mwa Waisraeli au mgeni anayekaa miongoni mwenu, akimtoa sadaka mtoto wake yeyote kwa mungu Moleki ni lazima mtu huyo auawe. Wananchi wa hapo watamuua kwa kumpiga mawe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waambie wana wa Isiraeli: Mtu ye yote, kama ni mwana wa Isiraeli au kama ni mgeni akaaye ugenini kwao Waisiraeli atakayetoa hata mmoja tu miongoni mwao walio wa uzao wake na kumpa Moloki sharti auawe, watu wa nchi hiyo sharti wamtupie mawe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena uwaambie wana wa Israeli, Mtu awaye yote miongoni mwa wana wa Israeli, au miongoni mwa wageni waketio katika Israeli, atakayetoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, sharti atauawa; wenyeji wa nchi watampiga kwa mawe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uwaambie Waisraeli hivi: Mutu yeyote kati ya Waisraeli au mugeni anayekaa kati yenu, akimutoa mutoto wake yeyote kuwa sadaka kwa mungu Moleki, mutu huyu anapaswa kuuawa. Wanainchi wa pale watamwua kwa kumupiga mawe.