Leviticus 21:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kuhani mkuu yeyote, kwa kuwa yeye ni mkuu kati ya ndugu zake, naye amemiminiwa mafuta ya kupaka kichwani pake, na kuwekwa wakfu ili ayavae mavazi matakatifu, asiache nywele zake kuwa ovyo wala asirarue mavazi yake kuomboleza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Kuhani mkuu, yule miongoni mwa ndugu zake ambaye amekwisha kupakwa mafuta kwa kumiminiwa juu ya kichwa chake, na ambaye amewekwa wakfu kuvaa mavazi ya ukuhani, kamwe asiache nywele zake bila kufunikwa, wala asirarue nguo zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na yeye aliye kuhani mkuu katika nduguze, ambaye mafuta ya kutiwa yamemiminwa kichwani mwake, naye akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kuhani mkuu yeyote, kwa kuwa yeye ni mkuu kati ya ndugu zake, naye amemiminiwa mafuta ya kupaka kichwani pake, na kuwekwa wakfu ili ayavae mavazi matakatifu, asiache nywele zake kuwa ovyo wala asirarue mavazi yake kuomboleza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Kuhani mkuu, aliye miongoni mwa ndugu zake, ambaye amekwisha kutiwa mafuta kwa kumiminiwa juu ya kichwa chake na ambaye amewekwa wakfu kuvaa mavazi ya ukuhani, kamwe asiache nywele zake bila kufunikwa wala asirarue nguo zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Kuhani mkuu, yule miongoni mwa ndugu zake ambaye amekwisha kutiwa mafuta kwa kumiminiwa juu ya kichwa chake, na ambaye amewekwa wakfu kuvaa mavazi ya ukuhani, kamwe asiache nywele zake bila kufunikwa, wala asirarue nguo zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na yeye aliye kuhani mkuu katika nduguze, ambaye mafuta ya kutiwa yamemiminwa kichwani mwake, naye akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kuhani mkuu yeyote, kwa kuwa yeye ni mkuu kati ya ndugu zake, naye amemiminiwa mafuta ya kupaka kichwani pake, na kuwekwa wakfu ili ayavae mavazi matakatifu, asiache nywele zake kuwa ovyo wala asirarue mavazi yake kuomboleza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye aliye mtambikaji mkuu miongoni mwa ndugu zake aliyemiminiwa kichwani pake mafuta ya kumpaka, aliyejazwa gao lake, apate kuyavaa yale mavazi yampasayo, asiziache wazi nywele za kichwani pake, wala asizirarue nguo zake,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na yeye aliye kuhani mkuu katika nduguze, ambaye mafuta ya kutiwa yamemiminwa kichwani mwake, naye akawekwa wakfu ili ayavae hayo mavazi, yeye hataziacha wazi nywele za kichwa chake, wala hatazirarua nguo zake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuhani Mukubwa ni mukubwa kati ya wandugu zake, naye amemiminiwa mafuta ya kupakaa juu ya kichwa chake, na kutakaswa kusudi avae nguo takatifu. Asiache nywele zake kuwa ovyo wala asipasue nguo zake kwa kuomboleza.