Leviticus 22:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kama binti yake kuhani ni mjane au amepewa talaka na hana mtoto, naye amerudi nyumbani kwa baba yake, akakaa naye kama alipokuwa kijana, basi, anaweza kula chakula cha baba yake. Hata hivyo, mgeni haruhusiwi kula vyakula hivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ikiwa binti ya kuhani amekuwa mjane au amepewa talaka, naye hana watoto, na akarudi kuishi na jamaa ya baba yake kama wakati wa usichana wake, binti huyo anaweza kula chakula cha baba yake. Hata hivyo, mtu asiyeruhusiwa hawezi kula chochote katika chakula hiki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kwamba binti ya kuhani ni mjane, au kwamba ameachwa na mumewe, wala hana mtoto, kisha amerudi na kuketi katika nyumba ya baba yake, kama vile katika ujana wake, yeye atakula katika chakula cha baba yake; lakini mgeni awaye yote asile katika chakula hicho.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kama binti yake kuhani ni mjane au amepewa talaka na hana mtoto, naye amerudi nyumbani kwa baba yake, akakaa naye kama alipokuwa kijana, basi, anaweza kula chakula cha baba yake. Hata hivyo, mgeni haruhusiwi kula vyakula hivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ikiwa binti wa kuhani amekuwa mjane au amepewa talaka, naye hana watoto, naye akarudi kuishi na jamaa ya baba yake kama wakati wa usichana wake, binti huyo anaweza kula chakula cha baba yake. Hata hivyo, mtu asiyeruhusiwa hawezi kula cho chote katika chakula hiki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ikiwa binti wa kuhani amekuwa mjane au amepewa talaka, naye hana watoto, na akarudi kuishi na jamaa ya baba yake kama wakati wa usichana wake, binti huyo anaweza kula chakula cha baba yake. Hata hivyo, mtu asiyeruhusiwa hawezi kula chochote katika chakula hiki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini ikiwa binti ya kuhani ni mjane, au ameachwa na mumewe, wala hana mtoto, kisha amerudi na kuishi katika nyumba ya baba yake, kama vile katika ujana wake, yeye atakula katika chakula cha baba yake; lakini mgeni yeyote asile katika chakula hicho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kama binti yake kuhani ni mjane au amepewa talaka na hana mtoto, naye amerudi nyumbani kwa baba yake, akakaa naye kama alipokuwa kijana, basi, anaweza kula chakula cha baba yake. Hata hivyo, mgeni haruhusiwi kula vyakula hivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini binti mtambikaji atakapokuwa mjane au atakapofukuzwa na mumewe hakuzaa watoto, kisha akirudi kukaa nymbani mwa baba yake, kama akiwa alivyokaa katika ujana wake, ataweza kukila chakula cha baba yake; lakini mgeni ye yote asikile.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kwamba binti ya kuhani ni mjane, au kwamba ameachwa na mumewe, wala hana mtoto, kisha amerudi na kuketi katika nyumba ya baba yake, kama vile katika ujana wake, yeye atakula katika chakula cha baba yake; lakini mgeni awaye yote asile katika chakula hicho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama binti ya kuhani ni mujane au amefukuzwa na mume wake na hana mutoto, naye amerudi kwa baba yake na kukaa naye kama vile alipokuwa kijana, basi, anaweza kula chakula cha baba yake. Hata hivyo, mugeni haruhusiwi kula chakula hicho.