Leviticus 22:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mwambie Aroni na wanawe makuhani na Waisraeli wote hivi: Kama mtu yeyote miongoni mwenu au mgeni yeyote aishiye katika Israeli akitoa sadaka yake, iwe ni ya kutimiza nadhiri au sadaka ya hiari ya kumtolea Mwenyezi-Mungu kwa kuteketezwa,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sema na Haruni na wanawe, na Waisraeli wote uwaambie: ‘Ikiwa mmoja wenu, aliye Mwisraeli au mgeni anayeishi katika nchi ya Israeli, atatoa matoleo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa Mwenyezi Mungu, iwe kutimiza nadhiri au kuwa sadaka ya hiari,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nena na Haruni na wanawe, na wana wa israeli wote, uwaambie, Mtu ye yote wa nyumba ya Israeli, au wa wageni walio katika Israeli, atakayetoa matoleo yake, kama ni nadhiri zao mojawapo, au kama ni sadaka yo yote ya hiari, watakayomtolea Bwana kuwa sadaka ya kuteketezwa;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mwambie Aroni na wanawe makuhani na Waisraeli wote hivi: Kama mtu yeyote miongoni mwenu au mgeni yeyote aishiye katika Israeli akitoa sadaka yake, iwe ni ya kutimiza nadhiri au sadaka ya hiari ya kumtolea Mwenyezi-Mungu kwa kuteketezwa,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sema na Aroni, wanawe na Waisraeli wote na uwaambie: ‘Ikiwa mmoja wenu, aliye Mwisraeli au mgeni anayeishi katika nchi ya Israeli, atatoa matoleo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa BWANA, iwe kutimiza nadhiri au kuwa sadaka ya hiari,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sema na Haruni na wanawe, na Waisraeli wote uwaambie: ‘Ikiwa mmoja wenu, aliye Mwisraeli au mgeni anayeishi katika nchi ya Israeli, atatoa matoleo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa bwana, iwe kutimiza nadhiri au kuwa sadaka ya hiari,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nena na Haruni na wanawe, na wana wa Israeli wote, uwaambie, Mtu yeyote wa nyumba ya Israeli, au wa wageni walio katika Israeli, atakayetoa matoleo yake, kama ni mojawapo ya nadhiri zao, au kama ni sadaka yoyote ya hiari, watakayomtolea BWANA kuwa sadaka ya kuteketezwa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mwambie Aroni na wanawe makuhani na Waisraeli wote hivi: Kama mtu yeyote miongoni mwenu au mgeni yeyote aishiye katika Israeli akitoa sadaka yake, iwe ni ya kutimiza nadhiri au sadaka ya hiari ya kumtolea Mwenyezi-Mungu kwa kuteketezwa,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sema na Haroni na wanawe na wana wote wa Isiraeli na kuwaambia: Mtu ye yote, kama ni wa mlango wa Isiraeli, au kama ni mgeni akaaye kwao Waisiraeli, akitaka kutoa toleo lake, kama ni la kulipa yo yote, aliyoyaapa, au kama ni kwa kupendezwa tu, basi, mtu akitaka kumtolea Bwana ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nena na Haruni na wanawe, na wana wa israeli wote, uwaambie, Mtu ye yote wa nyumba ya Israeli, au wa wageni walio katika Israeli, atakayetoa matoleo yake, kama ni nadhiri zao mojawapo, au kama ni sadaka yo yote ya hiari, watakayomtolea BWANA kuwa sadaka ya kuteketezwa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umwambie Haruni na wana wake makuhani na Waisraeli wote hivi: Kama mutu yeyote kati yenu au mugeni yeyote anayeishi katika Israeli akitoa sadaka yake, ikuwe ni ya kutimiza kiapo au sadaka ya mapenzi ya kumutolea Yawe kwa kuteketezwa,