Leviticus 22:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu yeyote anapomtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya amani ili kutimiza nadhiri au sadaka ya hiari kutoka katika kundi lake la mifugo, ili akubaliwe ni lazima awe ni mnyama mkamilifu; mnyama huyo asiwe na dosari yoyote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu yeyote aletapo sadaka ya amani kwa Mwenyezi Mungu kutoka kundi la ng’ombe au la mbuzi ili kutimiza nadhiri maalum au sadaka ya hiari, lazima sadaka hiyo isiwe na dosari au waa ili ikubalike.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mtu awaye yote atakayemtolea Bwana dhabihu katika sadaka za amani, ili kuondoa nadhiri, au sadaka ya moyo wa kupenda, katika ng'ombe, au katika kondoo, atakuwa mkamilifu, apate kukubaliwa; pasiwe na kilema ndani yake cho chote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu yeyote anapomtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya amani ili kutimiza nadhiri au sadaka ya hiari kutoka katika kundi lake la mifugo, ili akubaliwe ni lazima awe ni mnyama mkamilifu; mnyama huyo asiwe na dosari yoyote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu ye yote aletapo sadaka ya amani kwa BWANA kutoka kundi la ng'ombe au mbuzi ili kutimiza nadhiri maalum au sadaka ya hiari, lazima sadaka hiyo isiwe na dosari au waa ili ikubalike.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu yeyote aletapo sadaka ya amani kwa bwana kutoka kundi la ng’ombe au mbuzi ili kutimiza nadhiri maalum au sadaka ya hiari, lazima sadaka hiyo isiwe na dosari au waa ili ikubalike.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mtu yeyote atakayemtolea BWANA dhabihu katika sadaka za amani, ili kuondoa nadhiri, au sadaka ya moyo wa kupenda, katika ng'ombe, au katika kondoo, atakuwa mkamilifu, apate kukubaliwa; pasiwe na kilema chochote ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu yeyote anapomtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya amani ili kutimiza nadhiri au sadaka ya hiari kutoka katika kundi lake la mifugo, ili akubaliwe ni lazima awe ni mnyama mkamilifu; mnyama huyo asiwe na dosari yoyote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata mtu akitaka kumtolea Bwana ng'ombe ya tambiko ya shukrani, kama ni ya kuyalipa aliyoyaapa, au kama ni ya kupenda kwa moyo tu, kama anatoa ng'ombe au kama anatoa mbuzi au kondoo, sharti awe pasipo kilema, apate kupendeza, asiwe nyama mwenye kilema cho chote,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mtu awaye yote atakayemtolea BWANA dhabihu katika sadaka za amani, ili kuondoa nadhiri, au sadaka ya moyo wa kupenda, katika ng’ombe, au katika kondoo, atakuwa mkamilifu, apate kukubaliwa; pasiwe na kilema ndani yake cho chote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yeyote anapomutolea Yawe sadaka ya amani kwa kutimiza kiapo au sadaka ya mapenzi kutoka katika kundi lake la mifugo, kusudi akubaliwe anapaswa kuwa nyama mukamilifu, nyama huyo asikuwe na kilema chochote.