Leviticus 22:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Fahali au mwanakondoo aliye na kiungo kimoja kirefu au kifupi kuliko kawaida waweza kumtoa sadaka ya hiari; lakini huyo usimtoe kuwa sadaka ya kutimiza nadhiri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini unaweza ukamtoa ng’ombe au kondoo mwenye kilema au aliyedumaa kuwa sadaka ya hiari, lakini hii haitakubalika kuwa sadaka ya kutimiza nadhiri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ng'ombe, au mwana-kondoo aliye na kitu kilichozidi, au aliyepungukiwa na kitu katika vitu vya mwilini mwake, mna ruhusa kutoa kuwa sadaka ya moyo wa kupenda; lakini kwa ajili ya nadhiri hatakubaliwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Fahali au mwanakondoo aliye na kiungo kimoja kirefu au kifupi kuliko kawaida waweza kumtoa sadaka ya hiari; lakini huyo usimtoe kuwa sadaka ya kutimiza nadhiri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pengine, waweza kuamua na ukatoa sadaka ya hiari ng'ombe au kondoo mwenye kilema au aliyedumaa, lakini hii haitakubalika ili kuwa sadaka ya kutimiza nadhiri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini waweza ukatoa ng’ombe au kondoo mwenye kilema au aliyedumaa kama sadaka ya hiari, lakini hii haitakubalika kuwa sadaka ya kutimiza nadhiri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ng'ombe, au mwana-kondoo aliye na kitu kilichozidi, au aliyepungukiwa na kitu katika vitu vya mwilini mwake, mna ruhusa kutoa kuwa sadaka ya moyo wa kupenda; lakini kwa ajili ya nadhiri hatakubaliwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Fahali au mwanakondoo aliye na kiungo kimoja kirefu au kifupi kuliko kawaida waweza kumtoa sadaka ya hiari; lakini huyo usimtoe kuwa sadaka ya kutimiza nadhiri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ng'ombe au kondoo mwenye viungo virefu zaidi au mwenye viungo vifupi zaidi utaweza kumtoa ukipenda mwenyewe kwa moyo, lakini haitafaa kumtoa kuwa wa kuyalipa uliyoyaapa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ng’ombe, au mwana-kondoo aliye na kitu kilichozidi, au aliyepungukiwa na kitu katika vitu vya mwilini mwake, mna ruhusa kutoa kuwa sadaka ya moyo wa kupenda; lakini kwa ajili ya nadhiri hatakubaliwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ngombe dume au mwana-kondoo anayekuwa na kiungo kimoja kirefu au kifupi kuliko kawaida wanaweza kumutoa sadaka ya mapenzi. Lakini huyo usimutoe kuwa sadaka ya kutimiza kiapo.