Leviticus 22:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnyama ambaye kiungo chake cha kiume kimejeruhiwa, kimepondwa, kimevunjwa au kimekatwa, kamwe usimtolee Mwenyezi-Mungu; usifanye kitu cha namna hiyo nchini mwako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kamwe usimtolee Mwenyezi Mungu mnyama ambaye mapumbu yake yamejeruhiwa, au kuhasiwa, au kuraruliwa au kukatwa. Kamwe usifanye hivi katika nchi yako mwenyewe,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mnyama aliyeumia mapumbu yake, au kusetwa, au kuvunjwa, au kukatwa, msimtolee Bwana; wala msifanye hivi katika nchi yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnyama ambaye kiungo chake cha kiume kimejeruhiwa, kimepondwa, kimevunjwa au kimekatwa, kamwe usimtolee Mwenyezi-Mungu; usifanye kitu cha namna hiyo nchini mwako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kamwe usimtolee BWANA mnyama ambaye mapumbu yake yamejeruhiwa, au aliyehasiwa, au yaliyoraruliwa au kukatwa. Kamwe usifanye katika nchi yako mwenyewe,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kamwe usimtolee bwana mnyama ambaye mapumbu yake yamejeruhiwa, au kuhasiwa, au kuraruliwa au kukatwa. Kamwe usifanye hivi katika nchi yako mwenyewe,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mnyama aliyeumia mapumbu yake, au kusetwa, au kuvunjwa, au kukatwa, msimtolee BWANA; wala msifanye hivi katika nchi yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnyama ambaye kiungo chake cha kiume kimejeruhiwa, kimepondwa, kimevunjwa au kimekatwa, kamwe usimtolee Mwenyezi-Mungu; usifanye kitu cha namna hiyo nchini mwako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nyama mwenye mapumbu yaliyopondwa au yaliyosetwa au yaliyovunjwavunjwa au nyama aliyekatwa mapumbu kabisa msimtolee Bwana. Mtakapofika katika nchi yenu msivifanye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mnyama aliyeumia mapumbu yake, au kusetwa, au kuvunjwa, au kukatwa, msimtolee BWANA; wala msifanye hivi katika nchi yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyama ambaye kiungo chake cha uzazi kimeumizwa, kimepondwa, kimevunjwa au kimekatwa, usimutolee Yawe wala kumutoa kama vile sadaka katika inchi yako.