Leviticus 22:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waambie hivi: Kama mmoja wa wazawa wenu katika vizazi vyenu vyote atavikaribia vitu vitakatifu ambavyo Waisraeli wameviweka wakfu kwangu mimi Mwenyezi-Mungu akiwa najisi, mtu huyo atatengwa nami. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Waambie: ‘Katika vizazi vijavyo, ikiwa yeyote wa wazao wako ni najisi, naye akakaribia sadaka takatifu zile Waisraeli wanazoweka wakfu kwa Mwenyezi Mungu, mtu huyo lazima akatiliwe mbali na uso wangu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Waambie, Mtu ye yote wa kizazi chenu chote katika vizazi vyenu, atakayevikaribia vile vitu vitakatifu, ambavyo wana wa Israeli wamtakasia Bwana, naye ana unajisi, mtu huyo atakatiliwa mbali asiwe mbele zangu; mimi ndimi Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waambie hivi: Kama mmoja wa wazawa wenu katika vizazi vyenu vyote atavikaribia vitu vitakatifu ambavyo Waisraeli wameviweka wakfu kwangu mimi Mwenyezi-Mungu akiwa najisi, mtu huyo atatengwa nami. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Waambie: ‘Katika vizazi vijavyo, ikiwa ye yote wa wazao wako ni najisi kwa taratibu za kiibada, naye akakaribia sadaka takatifu Waisraeli wanazoziweka wakfu kwa BWANA, mtu huyo lazima akatiliwe mbali na uso wangu. Mimi ndimi BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Waambie: ‘Katika vizazi vijavyo, ikiwa yeyote wa wazao wako ni najisi kwa taratibu za kiibada, naye akakaribia sadaka takatifu zile Waisraeli wanazoweka wakfu kwa bwana, mtu huyo lazima akatiliwe mbali na uso wangu. Mimi ndimi bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Waambie, Mtu yeyote wa kizazi chenu chote katika vizazi vyenu, atakayevikaribia vile vitu vitakatifu, ambavyo wana wa Israeli wamtakasia BWANA, naye ana unajisi, mtu huyo atatengwa asiwe mbele zangu; mimi ndimi BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waambie hivi: Kama mmoja wa wazawa wenu katika vizazi vyenu vyote atavikaribia vitu vitakatifu ambavyo Waisraeli wameviweka wakfu kwangu mimi Mwenyezi-Mungu akiwa najisi, mtu huyo atatengwa nami. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waambie: Hivi vinavipasa vizazi vyenu vitakavyokuwa: mtu ye yote aliye wa uzao wenu wo wote akavifikia karibu vipaji vitakatifu, wana wa Isiraeli wanavyomtolea Bwana kuwa vitakatifu vyake, basi, akivikaribia na kuwa mwenye uchafu, sharti ang'olewe, atoweke usoni pangu; mimi ni Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Waambie, Mtu ye yote wa kizazi chenu chote katika vizazi vyenu, atakayevikaribia vile vitu vitakatifu, ambavyo wana wa Israeli wamtakasia BWANA, naye ana unajisi, mtu huyo atakatiliwa mbali asiwe mbele zangu; mimi ndimi BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uwaambie hivi: Kama mumoja wa wazao wenu katika vizazi vyenu vyote akikaribia vitu vitakatifu ambavyo Waisraeli wamevitakasa kwa ajili yangu mimi Yawe akiwa muchafu, mutu huyu atatengwa nami. Mimi ni Yawe.