Leviticus 22:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu yeyote wa nasaba ya Aroni akiwa na ugonjwa wa ukoma au anatokwa usaha asile vitu vitakatifu mpaka atakapokuwa safi. Mtu yeyote akimgusa mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti au mtu aliyetokwa na shahawa,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Ikiwa mzao wa Haruni ana ugonjwa wa ngozi unaoambukiza au anatokwa na usaha mwilini, hawezi kula sadaka takatifu hadi atakasike. Pia atakuwa najisi akigusa kitu chochote kilicho najisi kutokana na kugusa maiti, au akigusa mtu aliyetokwa na shahawa,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu ye yote wa kizazi cha Haruni aliye mwenye ukoma, au mwenye kisonono; yeye asile katika vitu vitakatifu, hata atakapokuwa safi. Tena mtu awaye yote atakayekinusa kitu kilicho na unajisi kwa sababu ya wafu, au mtu ambaye shahawa humtoka;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu yeyote wa nasaba ya Aroni akiwa na ugonjwa wa ukoma au anatokwa usaha asile vitu vitakatifu mpaka atakapokuwa safi. Mtu yeyote akimgusa mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti au mtu aliyetokwa na shahawa,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Ikiwa mzao wa Aroni ana ugonjwa wa ngozi unaoambukiza au anatokwa na usaha mwilini, hawezi kula sadaka takatifu mpaka atakasike. Vile vile atakuwa najisi ikiwa atagusa kitu cho chote kilichotiwa unajisi kwa kugusa maiti au mtu aliyetokwa na shahawa,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Ikiwa mzao wa Haruni ana ugonjwa wa ngozi unaoambukiza au anatokwa na usaha mwilini, hawezi kula sadaka takatifu mpaka atakasike. Pia atakuwa najisi ikiwa atagusa kitu chochote kilicho najisi kwa kugusa maiti au mtu aliyetokwa na shahawa,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu yeyote wa kizazi cha Haruni aliye na ukoma, au kisonono; asile katika vitu vitakatifu, hata atakapokuwa safi. Tena mtu yeyote atakayekinusa kitu kilicho na unajisi kwa sababu ya wafu, au mtu ambaye shahawa humtoka;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu yeyote wa nasaba ya Aroni akiwa na ugonjwa wa ukoma au anatokwa usaha asile vitu vitakatifu mpaka atakapokuwa safi. Mtu yeyote akimgusa mtu aliyetiwa unajisi kwa kugusa maiti au mtu aliyetokwa na shahawa,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu ye yote aliye wa uzao wake Haroni akiwa mwenye ukoma au kisonono asile vipaji vitakatifu, mpaka atakapokuwa mwenye kutakata. Atakayegusa mtu aliyejipatia uchafu kwa mfu au aliyetokwa na mbegu alipolala usingizi,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu ye yote wa kizazi cha Haruni aliye mwenye ukoma, au mwenye kisonono; yeye asile katika vitu vitakatifu, hata atakapokuwa safi. Tena mtu awaye yote atakayekinusa kitu kilicho na unajisi kwa sababu ya wafu, au mtu ambaye shahawa humtoka;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yeyote wa kizazi cha Haruni akiwa na ugonjwa wa ukoma au anatokwa usaha asikule vitu vitakatifu mpaka atakapokuwa safi. Mutu yeyote akigusa mutu aliyejichafua kwa kugusa maiti au mutu aliyetokwa na mbegu za uzazi,