Leviticus 23:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyo mnapofanya ishara ya kutoa huo mganda mbele yangu mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa ya mwanakondoo dume wa mwaka mmoja asiye na dosari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku hiyo mtakapoinua huo mganda, lazima mtoe kwa Mwenyezi Mungu dhabihu ya kuteketezwa kwa moto ya mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiye na dosari,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na siku hiyo mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana-kondoo wa kiume mkamilifu wa mwaka wa kwanza awe sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyo mnapofanya ishara ya kutoa huo mganda mbele yangu mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa ya mwanakondoo dume wa mwaka mmoja asiye na dosari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku hiyo mtakapoinua huo mganda, lazima mtoe kwa BWANA dhabihu ya kuteketezwa kwa moto mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiye na dosari,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku hiyo mtakapoinua huo mganda, lazima mtoe kwa bwana dhabihu ya kuteketezwa kwa moto ya mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiye na dosari,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na siku hiyo mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana-kondoo dume wa mwaka mmoja asiye na dosari, awe sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hiyo mnapofanya ishara ya kutoa huo mganda mbele yangu mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa ya mwanakondoo dume wa mwaka mmoja asiye na dosari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena siku hiyo ya kuupitisha mganda wenu motoni sharti mtengeneze mwana kondoo wa mwaka mmoja asiye na kilema kuwa ng'ombe ya tambiko ya Bwana ya kuteketezwa nzima
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na siku hiyo mtakayoutikisa mganda, mtamsongeza mwana-kondoo wa kiume mkamilifu wa mwaka wa kwanza awe sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hiyo munapofanya kitambulisho cha kutoa huo muganda mbele yangu mutanitolea mimi Yawe sadaka ya kuteketezwa ya mwana-kondoo dume wa mwaka mumoja asiyekuwa na kilema.