Leviticus 23:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pamoja na sadaka hiyo, mtatoa sadaka ya nafaka ya kilo mbili za unga laini uliochanganywa na mafuta ambayo mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu kwa moto, na harufu yake itanipendeza. Sadaka yake ya kinywaji ni lita moja ya divai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
pamoja na sadaka yake ya nafaka ya sehemu mbili za kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta, sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa kuteketezwa kwa moto; hii itakuwa sadaka iliyo harufu nzuri ya kupendeza, na sadaka yake ya kinywaji ya robo ya hini ya divai.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa Bwana kwa moto kuwa harufu ya kupendeza; na sadaka yake ya kinywaji itakuwa ni divai, robo ya hini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pamoja na sadaka hiyo, mtatoa sadaka ya nafaka ya kilo mbili za unga laini uliochanganywa na mafuta ambayo mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu kwa moto, na harufu yake itanipendeza. Sadaka yake ya kinywaji ni lita moja ya divai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
pamoja na sadaka ya unga laini wa nafaka sehemu mbili za kumi za efa uliochanganywa na mafuta, sadaka iliyotolewa kwa BWANA kwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kupendeza, na sadaka ya kinywaji robo ya hini ya divai.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
pamoja na sadaka yake ya nafaka ya sehemu mbili za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta, sadaka iliyotolewa kwa bwana kwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kupendeza, na sadaka yake ya kinywaji ya robo ya hini ya divai.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto kuwa harufu ya kupendeza; na sadaka yake ya kinywaji itakuwa ni divai, robo ya hini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pamoja na sadaka hiyo, mtatoa sadaka ya nafaka ya kilo mbili za unga laini uliochanganywa na mafuta ambayo mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu kwa moto, na harufu yake itanipendeza. Sadaka yake ya kinywaji ni lita moja ya divai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
pamoja na vilaji vyake vya tambiko: pishi moja ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta wa kumteketezea Bwana kuwa mnuko wa kumpendeza, tena kibaba kimoja cha mvinyo kuwa kinywaji chake cha tambiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto kuwa harufu ya kupendeza; na sadaka yake ya kinywaji itakuwa ni divai, robo ya hini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pamoja na sadaka hiyo, mutatoa sadaka ya vyakula ya kilo mbili za unga laini uliochanganywa na mafuta ambayo mutanitolea mimi Yawe kwa moto, na harufu yake itanipendeza. Sadaka yake ya kinywaji ni litre moja ya divai.