Leviticus 23:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kabla ya siku hiyo ya kuniletea mimi Mungu wenu sadaka hiyo, hamruhusiwi kula mazao ya kwanza ya mavuno yenu, yawe mabichi, yamekaangwa au yemeokwa kuwa mikate. Hili ni sharti la kufuata milele katika vizazi vyenu mahali popote mtakapoishi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kamwe msile mkate wowote, au nafaka iliyokaangwa au nafaka mpya, hadi siku ile mtakayomletea Mungu wenu sadaka hii. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo, popote mnapoishi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi msile mkate, wala bisi, wala masuke machanga, hata siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kabla ya siku hiyo ya kuniletea mimi Mungu wenu sadaka hiyo, hamruhusiwi kula mazao ya kwanza ya mavuno yenu, yawe mabichi, yamekaangwa au yemeokwa kuwa mikate. Hili ni sharti la kufuata milele katika vizazi vyenu mahali popote mtakapoishi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kamwe msile mkate wo wote, au nafaka iliyokaangwa au nafaka mpya, mpaka siku ile mtakayomletea Mungu wako sadaka hii. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo po pote mnapoishi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kamwe msile mkate wowote, au nafaka iliyokaangwa au nafaka mpya, mpaka siku ile mtakayomletea Mungu wenu sadaka hii. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo, popote mnapoishi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi msile mkate, bisi, au masuke machanga, hata siku hiyo hiyo, hadi mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kabla ya siku hiyo ya kuniletea mimi Mungu wenu sadaka hiyo, hamruhusiwi kula mazao ya kwanza ya mavuno yenu, yawe mabichi, yamekaangwa au yemeokwa kuwa mikate. Hili ni sharti la kufuata milele katika vizazi vyenu mahali popote mtakapoishi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Msile mikate ya ngano mpya wala bisi wala chenga za masuke machanga mpaka siku hiyo, mtakapomtolea Mungu wenu vipaji hivyo vya tambiko. Maongozi haya na yawe ya kale na kale kwa vizazi vyenu po pote, mtakapokaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi msile mkate, wala bisi, wala masuke machanga, hata siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mbele ya siku hiyo ya kuniletea mimi Mungu wenu sadaka hiyo, hamuruhusiwi kula mazao ya kwanza ya mavuno yenu, yakuwe mabichi, yamekaangwa au yemepikwa kuwa mikate. Hili ni sharti la kufuata siku zote katika vizazi vyenu pahali popote mutakapoishi.