Leviticus 23:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnamo siku ya hamsini, siku ya pili ya Sabato ya saba, mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka ya nafaka mpya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtahesabu siku hamsini hadi siku inayofuata Sabato ya saba, ndipo mtatoa sadaka ya nafaka mpya kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
hata siku ya pili ya hiyo Sabato ya saba mtahesabu siku hamsini; nanyi mtamsongezea Bwana sadaka ya unga mpya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnamo siku ya hamsini, siku ya pili ya Sabato ya saba, mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka ya nafaka mpya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtahesabu mpaka siku inayofuata Sabato ya saba, siku hamsini, ndipo mtatoa sadaka ya nafaka mpya kwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtahesabu siku hamsini mpaka siku inayofuata Sabato ya saba, ndipo mtatoa sadaka ya nafaka mpya kwa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
hata siku ya pili ya hiyo Sabato ya saba mtahesabu siku hamsini; nanyi mtamsongezea BWANA sadaka ya unga mpya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnamo siku ya hamsini, siku ya pili ya Sabato ya saba, mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka ya nafaka mpya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
siku zao, mtakazozihesabu mpaka kesho yake siku ya mapumziko ya saba ni siku 50; zikitimia, ndipo mmtolee Bwana vilaji vipya vya tambiko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
hata siku ya pili ya hiyo Sabato ya saba mtahesabu siku hamsini; nanyi mtamsongezea BWANA sadaka ya unga mpya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku ya makumi tano, siku ya pili ya Sabato ya saba, mutanitolea mimi Yawe sadaka ya vyakula vipya.