Leviticus 23:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila jamaa italeta mikate miwili ya sadaka ya kutoa kwa ishara mbele yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Kila mkate ni lazima uwe umetengenezwa kwa kilo mbili za unga laini uliotiwa chachu; na huo mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu ukiwa ni matoleo ya malimbuko yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutoka popote mnapoishi, mtaleta mikate miwili iliyotengenezwa kwa sehemu mbili za kumi ya efa moja ya unga laini, uliookwa kwa chachu, kuwa sadaka ya kuinuliwa ya malimbuko kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila jamaa italeta mikate miwili ya sadaka ya kutoa kwa ishara mbele yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Kila mkate ni lazima uwe umetengenezwa kwa kilo mbili za unga laini uliotiwa chachu; na huo mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu ukiwa ni matoleo ya malimbuko yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka po pote mnapoishi, leteni mikate miwili iliyookwa kwa unga laini, sehemu mbili za kumi za efa uliookwa wenye chachu, kuwa sadaka ya kuinuliwa ya malimbuko kwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka popote mnapoishi, mtaleta mikate miwili ya unga laini, sehemu mbili za kumi za efa, uliookwa kwa chachu, kuwa sadaka ya kuinuliwa ya malimbuko kwa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila jamaa italeta mikate miwili ya sadaka ya kutoa kwa ishara mbele yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Kila mkate ni lazima uwe umetengenezwa kwa kilo mbili za unga laini uliotiwa chachu; na huo mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu ukiwa ni matoleo ya malimbuko yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Makaoni mwenu mtoe mikate miwili ya kupitishwa motoni iliyotengenezwa kwa pishi moja ya unga mwembamba, iliyookwa ilipokwisha kuchachuka, ipate kuwa malimbuko ya Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila jamaa italeta mikate miwili ya sadaka ya kutoa kwa kitambulisho mbele yangu mimi Yawe. Kila mukate utatengenezwa kwa kilo mbili za unga laini uliotiwa chachu na huo mutanitolea mimi Yawe ukiwa ni matoleo ya malimbuko yenu.