Leviticus 23:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Unapovuna mavuno yako shambani, kamwe usivune kabisa hadi mpakani mwa shamba lako wala usirudi nyuma kukusanya masalio. Utawaachia hayo maskini na wageni. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Mnapovuna mavuno ya ardhi yenu, msivune hadi mpakani mwa shamba lenu, au kukusanya masazo ya mavuno yenu. Hayo utayaacha kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi hapo mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, usivune kabisa kabisa pembe za shamba lako, wala msiyakusanye masazo ya mavuno yako; utayaacha kwa ajili ya huyo maskini, na mgeni; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Unapovuna mavuno yako shambani, kamwe usivune kabisa hadi mpakani mwa shamba lako wala usirudi nyuma kukusanya masalio. Utawaachia hayo maskini na wageni. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Mnapovuna mavuno ya ardhi yenu, msivune hadi mpakani mwa shamba lenu au kukusanya masazo ya mavuno yenu. Hayo utayaacha kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimi BWANA Mungu wenu.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Mnapovuna mavuno ya ardhi yenu, msivune hadi mpakani mwa shamba lenu, au kukusanya masazo ya mavuno yenu. Hayo utayaacha kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimi bwana Mwenyezi Mungu wenu.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi hapo mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, msivune kabisa kabisa pembe za shamba lako, wala msiyakusanye masazo ya mavuno yako; utayaacha kwa ajili ya huyo maskini na mgeni; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Unapovuna mavuno yako shambani, kamwe usivune kabisa hadi mpakani mwa shamba lako wala usirudi nyuma kukusanya masalio. Utawaachia hayo maskini na wageni. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtakapovuna mavuno ya nchi yenu msikate napo pembeni penye mashamba yenu kupavunia napo, wala msiokoteze viokotezo vya mavuno yenu, ila mviache, viokotezwe na wakiwa na wageni. Mimi Bwana ni Mungu wenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi hapo mtakapovuna mavuno ya nchi yenu, usivune kabisa kabisa pembe za shamba lako, wala msiyakusanye masazo ya mavuno yako; utayaacha kwa ajili ya huyo maskini, na mgeni; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Unapovuna mavuno yako katika shamba, usivune kabisa mpaka kwenye mupaka wa shamba lako wala usirudi nyuma kukusanya mabaki. Utawaachia hayo wamasikini na wageni. Mimi ni Yawe, Mungu wenu.