Leviticus 23:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kutakuwa na siku sita za kufanya kazi. Lakini siku ya saba ni Sabato; siku hiyo ni ya mapumziko rasmi, hamtafanya kazi na mtakuwa na mkutano mtakatifu. Siku hiyo ya saba hamtafanya kazi; hiyo ni Sabato ambayo ni wakfu kwangu mimi Mwenyezi-Mungu katika makao yenu yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Kuna siku sita mnazoweza kufanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika, siku ya kusanyiko takatifu. Hamtafanya kazi yoyote. Popote mnapoishi, ni Sabato kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, kusanyiko takatifu; msifanye kazi ya namna yo yote; ni Sabato kwa Bwana katika makao yenu yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kutakuwa na siku sita za kufanya kazi. Lakini siku ya saba ni Sabato; siku hiyo ni ya mapumziko rasmi, hamtafanya kazi na mtakuwa na mkutano mtakatifu. Siku hiyo ya saba hamtafanya kazi; hiyo ni Sabato ambayo ni wakfu kwangu mimi Mwenyezi-Mungu katika makao yenu yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Kuna siku sita mnazoweza kufanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika, siku ya kusanyiko takatifu. Hamtafanya kazi yo yote, po pote mnapoishi, ni Sabato kwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Kuna siku sita mnazoweza kufanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika, siku ya kusanyiko takatifu. Hamtafanya kazi yoyote. Popote mnapoishi, ni Sabato kwa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, kusanyiko takatifu; msifanye kazi ya namna yoyote; ni Sabato kwa BWANA katika makao yenu yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kutakuwa na siku sita za kufanya kazi. Lakini siku ya saba ni Sabato; siku hiyo ni ya mapumziko rasmi, hamtafanya kazi na mtakuwa na mkutano mtakatifu. Siku hiyo ya saba hamtafanya kazi; hiyo ni Sabato ambayo ni wakfu kwangu mimi Mwenyezi-Mungu katika makao yenu yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kazi sharti zifanywe siku sita, lakini siku ya saba ni siku ya kupumzika kabisa ya kukutania Patakatifu; hapo isifanywe kazi yo yote, maana ndiyo siku ya mapumziko ya kumheshimu Bwana katika makao yenu yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, kusanyiko takatifu; msifanye kazi ya namna yo yote; ni Sabato kwa BWANA katika makao yenu yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kutakuwa siku sita za kufanya kazi. Lakini siku ya saba ni Sabato. Siku hiyo ni ya mapumziko, hamutafanya kazi na mutakuwa na mukutano mutakatifu. Siku hiyo ya saba hamutafanya kazi. Hiyo ni Sabato ambayo ni takatifu kwangu mimi Yawe katika makao yenu yote.