Leviticus 23:32 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyo, itakuwa kwenu Sabato ya mapumziko rasmi na mtafunga. Siku ya Sabato ni siku ya kumi ya mwezi huo tangu jioni hadi jioni inayofuata.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni Sabato ya mapumziko kwenu, na lazima mfunge. Tangu jioni ya siku ya tisa ya mwezi hadi jioni inayofuata, mtaishika Sabato yenu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Itakuwa kwenu sabato ya kustarehe kabisa, nanyi mtazitesa nafsi zenu; siku ya kenda ya mwezi wakati wa jioni, tangu jioni hata jioni, mtaishika hiyo Sabato yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyo, itakuwa kwenu Sabato ya mapumziko rasmi na mtafunga. Siku ya Sabato ni siku ya kumi ya mwezi huo tangu jioni hadi jioni inayofuata.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni Sabato ya mapumziko kwenu ninyi, ni lazima mfunge. Tangu jioni ya siku ya tisa ya mwezi hadi jioni inayofuata, mtaishika Sabato yenu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni Sabato ya mapumziko kwenu ninyi, na lazima mfunge. Tangu jioni ya siku ya tisa ya mwezi hadi jioni inayofuata, mtaishika Sabato yenu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Itakuwa kwenu sabato ya kustarehe kabisa, nanyi mtajinyima; siku ya tisa ya mwezi wakati wa jioni, tangu jioni hadi jioni, mtaishika hiyo Sabato yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hiyo, itakuwa kwenu Sabato ya mapumziko rasmi na mtafunga. Siku ya Sabato ni siku ya kumi ya mwezi huo tangu jioni hadi jioni inayofuata.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Iwe kwenu siku ya mapumziko ya kupumzika kabisa ya kujitesa kwa kufunga. Sharti mpumzike jioni ile siku ya tisa ya mwezi huo toka hapo jioni, ikiwa jioni tena, mpumzike kwa kuishika hiyo siku yenu ya mapumziko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Itakuwa kwenu sabato ya kustarehe kabisa, nanyi mtazitesa nafsi zenu; siku ya kenda ya mwezi wakati wa jioni, tangu jioni hata jioni, mtaishika hiyo Sabato yenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hiyo, itakuwa kwenu Sabato ya mapumziko na mutafunga. Siku ya Sabato ni siku ya kumi ya mwezi huo tangu magaribi mpaka magaribi inayofuata.