Leviticus 23:36 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa muda wa siku saba mtatoa sadaka anazopewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Siku ya nane mtakuwa na mkutano mkubwa na kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa. Mkutano huo ni mtakatifu. Siku hiyo msifanye kazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa siku saba toeni sadaka kwa Mwenyezi Mungu za kuteketezwa kwa moto. Kwenye siku ya nane fanyeni kusanyiko takatifu, na kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa Mwenyezi Mungu. Ni kusanyiko la mwisho, msifanye kazi zenu za kawaida.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yo yote ya utumishi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa muda wa siku saba mtatoa sadaka anazopewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Siku ya nane mtakuwa na mkutano mkubwa na kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa. Mkutano huo ni mtakatifu. Siku hiyo msifanye kazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa siku saba toeni sadaka kwa BWANA za kuteketezwa kwa moto, kwenye siku ya nane fanyeni kusanyiko takatifu na mtoe sadaka kwa BWANA ya kuteketezwa kwa moto. Ni kusanyiko la mwisho, msifanye kazi zenu za kawaida.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa siku saba toeni sadaka kwa bwana za kuteketezwa kwa moto. Kwenye siku ya nane fanyeni kusanyiko takatifu, na mtoe sadaka kwa bwana ya kuteketezwa kwa moto. Ni kusanyiko la mwisho, msifanye kazi zenu za kawaida.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtamsogezea BWANA sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamtolea BWANA sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yoyote ya utumishi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa muda wa siku saba mtatoa sadaka anazopewa Mwenyezi-Mungu kwa moto. Siku ya nane mtakuwa na mkutano mkubwa na kumtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuteketezwa. Mkutano huo ni mtakatifu. Siku hiyo msifanye kazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku saba sharti mmtolee Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa; siku ya nane na mkutanie Patakatifu, mmtolee Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa, ni siku ya mkutano, kwa hiyo msifanye kazi yo yote ya utumishi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtamsongezea BWANA sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; nanyi mtamsongezea BWANA sadaka kwa moto; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yo yote ya utumishi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa muda wa siku saba mutatoa sadaka Yawe anazopewa kwa moto. Siku ya nane mutakuwa na mukutano mutakatifu na kumutolea Yawe sadaka ya kuteketezwa. Mukutano huo ni mutakatifu. Siku hiyo musifanye kazi.