Leviticus 23:40 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika siku ya kwanza mtachukua matunda ya miti yenu mizuri, matawi ya mitende, matawi yenye majani mengi na matawi ya miti iotayo kandokando ya mto, nanyi mtafanya sherehe mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu kwa siku saba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya kwanza mtachukua matunda mazuri ya miti, matawi ya mitende, matawi yenye majani mengi, na matawi ya mirebi, nanyi mtashangilia mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa siku saba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi siku ya kwanza mtajipatia matunda ya miti mizuri, na makuti ya mitende, na matawi ya miti minene, na mierebi ya vijitoni; nanyi mtafurahi mbele za Bwana, Mungu wenu, muda wa siku saba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika siku ya kwanza mtachukua matunda ya miti yenu mizuri, matawi ya mitende, matawi yenye majani mengi na matawi ya miti iotayo kandokando ya mto, nanyi mtafanya sherehe mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu kwa siku saba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwenye siku ya kwanza mtachukua matunda mazuri ya miti, matawi ya mitende, matawi yenye majani mengi, na matawi ya mirebi, nanyi mtashangilia mbele za BWANA Mungu wenu kwa siku saba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ya kwanza mtachukua matunda mazuri ya miti, matawi ya mitende, matawi yenye majani mengi, na matawi ya mirebi, nanyi mtashangilia mbele za bwana Mwenyezi Mungu wenu kwa siku saba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi siku ya kwanza mtajipatia matunda ya miti mizuri, na makuti ya mitende, na matawi ya miti minene, na mierezi ya vijitoni; nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, muda wa siku saba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika siku ya kwanza mtachukua matunda ya miti yenu mizuri, matawi ya mitende, matawi yenye majani mengi na matawi ya miti iotayo kandokando ya mto, nanyi mtafanya sherehe mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu kwa siku saba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena siku ya kwanza na mjipatie matunda mazuri ya miti na makuti mabichi ya mitende na matawi ya miti ya maporini na ya mitoni, mmfurahie Bwana Mungu wenu siku saba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi siku ya kwanza mtajipatia matunda ya miti mizuri, na makuti ya mitende, na matawi ya miti minene, na mierebi ya vijitoni; nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, muda wa siku saba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku ya kwanza mutatwaa matunda ya miti yenu mizuri, matawi ya ngazi, matawi yenye majani mengi na matawi ya miti inayoota kandokando ya muto, nanyi mutafanya sikukuu mbele ya Yawe, Mungu wenu kwa siku saba.