Leviticus 23:41 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mwaka ni lazima kuadhimisha sikukuu hii kwa muda wa siku saba kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu. Hili ni sharti la kufuata milele katika vizazi vyenu. Mtaifanya katika mwezi wa saba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtaadhimisha siku hii kuwa sikukuu kwa Mwenyezi Mungu kwa siku saba kila mwaka. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo; iadhimisheni mwezi wa saba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi mtaishika kuwa sikukuu kwa Bwana muda wa siku saba katika mwaka; ni amri ya milele katika vizazi vyenu; mtaishika katika mwezi wa saba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mwaka ni lazima kuadhimisha sikukuu hii kwa muda wa siku saba kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu. Hili ni sharti la kufuata milele katika vizazi vyenu. Mtaifanya katika mwezi wa saba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtaadhimisha siku hii kuwa sikukuu kwa BWANA kwa siku saba kila mwaka. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo; iadhimisheni kwenye mwezi wa saba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtaadhimisha siku hii kuwa sikukuu kwa bwana kwa siku saba kila mwaka. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo; iadhimisheni mwezi wa saba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi mtaishika kuwa sikukuu kwa BWANA muda wa siku saba katika mwaka; ni amri ya milele katika vizazi vyenu; mtaishika katika mwezi wa saba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila mwaka ni lazima kuadhimisha sikukuu hii kwa muda wa siku saba kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu. Hili ni sharti la kufuata milele katika vizazi vyenu. Mtaifanya katika mwezi wa saba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hiyo iliyo sikukuu ya Bwana sharti mwile kila mwaka siku saba. Maongozi haya na yawe ya kale na kale kwa vizazi vyenu, mwile sikukuu hii siku saba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi mtaishika kuwa sikukuu kwa BWANA muda wa siku saba katika mwaka; ni amri ya milele katika vizazi vyenu; mtaishika katika mwezi wa saba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mwaka munapaswa kufanya sikukuu hii kwa muda wa siku saba kwa heshima ya Yawe. Hili ni sharti la kufuata siku zote katika vizazi vyenu. Mutaifanya katika mwezi wa saba.