Leviticus 24:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja kukatokea mzozo huko kambini kati ya Mwisraeli mmoja na kijana mmoja wa mama Mwisraeli aitwaye Shelomithi lakini baba Mmisri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi mwana wa mama Mwisraeli na baba Mmisri alienda miongoni mwa Waisraeli, nayo mapigano yakatokea ndani ya kambi kati yake na Mwisraeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa mwana wa mwanamke wa Kiisraeli, ambaye babaye alikuwa Mmisri, akatokea kati ya wana wa Israeli; na huyo mwana wa mwanamke wa Kiisraeli, na Mwisraeli mmoja, wakapigana pamoja ndani ya marago;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja kukatokea mzozo huko kambini kati ya Mwisraeli mmoja na kijana mmoja wa mama Mwisraeli aitwaye Shelomithi lakini baba Mmisri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi mwana wa mama wa Kiisraeli ambaye baba yake ni Mmisri alikwenda miongoni mwa Waisraeli na mapigano yakatokea ndani ya kambi kati yake na Mwisraeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi mwana wa mama Mwisraeli na baba Mmisri alikwenda miongoni mwa Waisraeli, nayo mapigano yakatokea ndani ya kambi kati yake na Mwisraeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa mwanamume mmoja ambaye mama yake ni Mwisraeli, na babaye ni Mmisri, alitokea kati ya wana wa Israeli akalikufuru; na kupigana na Mwisraeli katika kambi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja kukatokea mzozo huko kambini kati ya Mwisraeli mmoja na kijana mmoja wa mama Mwisraeli aitwaye Shelomithi lakini baba Mmisri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, mwana wa mwanamke wa Kiisiraeli mwenye baba wa Kimisri alipotokea katikati ya wana wa Isiraeli, huyu mwana wa mwanamke wa Kiisiraeli akagombana na mtu wa Kiisiraeli makambini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa mwana wa mwanamke wa Kiisraeli, ambaye babaye alikuwa Mmisri, akatokea kati ya wana wa Israeli; na huyo mwana wa mwanamke wa Kiisraeli, na Mwisraeli mmoja, wakapigana pamoja ndani ya marago;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja kukatokea fujo kule katika kambi kati ya Mwisraeli mumoja na kijana mumoja wa mama Mwisraeli lakini baba Mumisri.