Leviticus 24:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja yule kijana ambaye mama yake aliitwa Shelomithi binti Dibri wa kabila la Dani, alilikufuru na kulilaani jina la Mungu. Basi watu walimpeleka kijana kwa Mose,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huyu mwana wa mwanamke Mwisraeli akalikufuru Jina la Mwenyezi Mungu kwa kulaani; kwa hiyo wakamleta kwa Musa. (Mama yake aliitwa Shelomithi binti Dibri, wa kabila la Dani.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kisha huyo mwana wa mwanamke wa Kiisraeli akalikufuru hilo Jina, na kuapiza; nao wakamleta kwa Musa. Na jina la mamaye alikuwa akiitwa Shelomithi, binti ya Dibri, wa kabila ya Dani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja yule kijana ambaye mama yake aliitwa Shelomithi binti Dibri wa kabila la Dani, alilikufuru na kulilaani jina la Mungu. Basi watu walimpeleka kijana kwa Mose,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huyu mwana wa mwanamke wa Kiisraeli akalikufuru Jina la BWANA na kulaani; kwa hiyo wakamleta kwa Mose. (Jina la mama yake aliitwa Shelomithi binti wa Dibri wa kabila la Dani.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huyu mwana wa mwanamke Mwisraeli akalikufuru Jina la bwana kwa kulaani; kwa hiyo wakamleta kwa Musa. (Jina la mama yake aliitwa Shelomithi binti wa Dibri, wa kabila la Dani.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kisha huyo mwanamume ambaye mama ni Mwisraeli akakufuru jina la Bwana na kulaani nao watu wakampeleka kwa Musa. Mama yake mtu huyo alikuwa akiitwa Shelomithi, binti ya Dibri, wa kabila la Dani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja yule kijana ambaye mama yake aliitwa Shelomithi binti Dibri wa kabila la Dani, alilikufuru na kulilaani jina la Mungu. Basi watu walimpeleka kijana kwa Mose,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye yule mwana wa mwanamke wa Kiisiraeli akalitukana Jina la Bwana pamoja na kuliapiza. Ndipo, walipompeleka kwa Mose, nalo jina la mama yake lilikuwa Selomiti, binti Diburi, wa shina la Dani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kisha huyo mwana wa mwanamke wa Kiisraeli akalikufuru hilo Jina, na kuapiza; nao wakamleta kwa Musa. Na jina la mamaye alikuwa akiitwa Shelomithi, binti ya Dibri, wa kabila ya Dani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule kijana ambaye mama yake aliitwa Selemoti binti ya Dibri wa kabila la Dani, alitukana Mungu na kuzarau jina lake. Basi watu wakamupeleka kijana kwa Musa,