Leviticus 24:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu yeyote awe ni mwenyeji au mgeni anayemkufuru Mwenyezi-Mungu, jumuiya nzima itamuua kwa kumpiga mawe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeyote atakayekufuru Jina la Mwenyezi Mungu ni lazima auawe. Kusanyiko lote watampiga kwa mawe. Iwe ni mgeni au mzawa, atakapolikufuru Jina la Mwenyezi Mungu, ni lazima auawe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na yeye atakayelikufuru jina la Bwana hakika atauawa; mkutano wote watamwua kwa kumpiga kwa mawe; kama ni mgeni, kama ni mzalia, hapo atakapolikufuru jina la Bwana atauawa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu yeyote awe ni mwenyeji au mgeni anayemkufuru Mwenyezi-Mungu, jumuiya nzima itamuua kwa kumpiga mawe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ye yote atakayekufuru Jina la BWANA ni lazima auawe. Kusanyiko lote litampiga kwa mawe. Iwapo ni mgeni au mzawa, atakapolikufuru Jina la BWANA, ni lazima auawe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
yeyote atakayekufuru Jina la bwana ni lazima auawe. Kusanyiko lote litampiga kwa mawe. Iwe ni mgeni au mzawa, atakapolikufuru Jina la bwana, ni lazima auawe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na yeyote atakayelaani jina la BWANA hakika atauawa; mkutano wote watamwua kwa kumpiga kwa mawe; kama ni mgeni, kama ni mzaliwa, hapo atakapolaani jina la BWANA atauawa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu yeyote awe ni mwenyeji au mgeni anayemkufuru Mwenyezi-Mungu, jumuiya nzima itamuua kwa kumpiga mawe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Atakayelitukana Jina la Bwana sharti auawe kabisa, watu wote wa mkutano huu wakimpiga mawe. Kama ni mgeni au kama ni mwenyeji, kwa kulitukana hilo Jina hana budi kuuawa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na yeye atakayelikufuru jina la BWANA hakika atauawa; mkutano wote watamwua kwa kumpiga kwa mawe; kama ni mgeni, kama ni mzalia, hapo atakapolikufuru jina la BWANA atauawa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu yeyote akuwe ni mwenyeji au mugeni anayemutukana Yawe, wote pamoja watamwua kwa kumupiga mawe.