Leviticus 24:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mose akawaambia Waisraeli hayo yote. Wakampeleka yule mtu aliyemlaani Mwenyezi-Mungu nje ya kambi, wakamuua kwa kumpiga mawe. Ndivyo Waisraeli walivyofanya kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Musa akasema na Waisraeli, nao wakamchukua yule aliyekufuru nje ya kambi na kumpiga mawe. Waisraeli wakafanya kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akanena na wana wa Israeli, nao wakamtoa huyo aliyeapiza nje ya marago, wakamwua kwa kumpiga kwa mawe. Wana wa Israeli wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Musa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mose akawaambia Waisraeli hayo yote. Wakampeleka yule mtu aliyemlaani Mwenyezi-Mungu nje ya kambi, wakamuua kwa kumpiga mawe. Ndivyo Waisraeli walivyofanya kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Mose akasema na Waisraeli, nao wakamchukua yule aliyekufuru nje ya kambi na kumpiga mawe. Waisraeli wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Mose.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Musa akasema na Waisraeli, nao wakamchukua yule aliyekufuru nje ya kambi na kumpiga mawe. Waisraeli wakafanya kama bwana alivyomwagiza Musa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akanena na wana wa Israeli, nao wakamtoa huyo aliyeapiza nje ya kambi, wakamwua kwa kumpiga kwa mawe. Wana wa Israeli wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mose akawaambia Waisraeli hayo yote. Wakampeleka yule mtu aliyemlaani Mwenyezi-Mungu nje ya kambi, wakamuua kwa kumpiga mawe. Ndivyo Waisraeli walivyofanya kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mose alipokwisha kuwaambia wana wa Isiraeli maneno haya, wakamtokeza yule mwenye kutukana nje ya makambi, wakamwua kwa kumpiga mawe; wana wa Isiraeli wakafanya, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akanena na wana wa Israeli, nao wakamtoa huyo aliyeapiza nje ya marago, wakamwua kwa kumpiga kwa mawe. Wana wa Israeli wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Musa akawaambia Waisraeli hayo yote. Wakamupeleka yule mutu aliyelaani Yawe inje ya kambi, wakamwua kwa kumupiga mawe. Ndivyo Waisraeli walivyofanya kama vile Yawe alivyomwamuru Musa.