Leviticus 24:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aroni ataiweka taa hiyo ndani ya hema la mkutano, nje ya pazia la sanduku la maamuzi ili ipate kuwaka mbele yangu tangu usiku mpaka asubuhi. Hili ni sharti la kufuata milele katika vizazi vyenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nje ya pazia la Sanduku la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Haruni ataziwasha taa mbele za Mwenyezi Mungu kuanzia jioni hadi asubuhi daima. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hapo nje ya pazia la ushahidi, ndani ya hema ya kukutania, Haruni ataitengeza tangu jioni hata asubuhi mbele za Bwana daima; ni amri ya milele katika vizazi vyenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aroni ataiweka taa hiyo ndani ya hema la mkutano, nje ya pazia la sanduku la maamuzi ili ipate kuwaka mbele yangu tangu usiku mpaka asubuhi. Hili ni sharti la kufuata milele katika vizazi vyenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Aroni ataziwasha taa mbele za BWANA kuanzia jioni hadi asubuhi kwa mfululizo. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Haruni ataziwasha taa mbele za bwana kuanzia jioni hadi asubuhi bila kuzima. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hapo nje ya pazia la ushuhuda, ndani ya hema ya kukutania, Haruni ataitengeneza tangu jioni hadi asubuhi mbele za BWANA daima; ni amri ya milele katika vizazi vyenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aroni ataiweka taa hiyo ndani ya hema la mkutano, nje ya pazia la sanduku la maamuzi ili ipate kuwaka mbele yangu tangu usiku mpaka asubuhi. Hili ni sharti la kufuata milele katika vizazi vyenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo nje ya pazia penye Sanduku la Ushahidi katika Hema la Mkutano Haroni azitengeneze hizo taa, ziwake tangu jioni hata asubuhi mbele ya Bwana pasipo kukoma. Maongozi haya na yawe ya kale na kale kwa vizazi vyenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hapo nje ya pazia la ushahidi, ndani ya hema ya kukutania, Haruni ataitengeza tangu jioni hata asubuhi mbele za BWANA daima; ni amri ya milele katika vizazi vyenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haruni ataweka taa hiyo ndani ya hema la mukutano, inje ya pazia la Sanduku la Agano kusudi ipate kuwaka mbele yangu tangu usiku mpaka asubui. Hili ni sharti la kufuata siku zote katika vizazi vyenu.