Leviticus 24:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aroni na wazawa wake peke yao ndio wanaoruhusiwa kula mikate hiyo kwani ni mitakatifu kabisa kwa sababu ni sehemu ya sadaka ninazotolewa mimi Mwenyezi-Mungu kwa moto. Hiyo ni haki yao milele.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hii ni mali ya Haruni na wanawe, watakaoila katika mahali patakatifu, kwa sababu ni sehemu takatifu sana ya fungu lao milele la sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa kuteketezwa kwa moto.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nayo itakuwa ya Haruni na wanawe; nao wataila katika mahali patakatifu; kwa sababu kwake ni takatifu sana katika sadaka zisongezwazo kwa Bwana kwa moto, kwa amri ya milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aroni na wazawa wake peke yao ndio wanaoruhusiwa kula mikate hiyo kwani ni mitakatifu kabisa kwa sababu ni sehemu ya sadaka ninazotolewa mimi Mwenyezi-Mungu kwa moto. Hiyo ni haki yao milele.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii ni mali ya Aroni na wanawe, watakaoila katika mahali patakatifu, kwa sababu ni sehemu takatifu sana ya fungu lao la kawaida la sadaka iliyotolewa kwa BWANA kwa kuteketezwa kwa moto.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hii ni mali ya Haruni na wanawe, watakaoila katika mahali patakatifu, kwa sababu ni sehemu takatifu sana ya fungu lao la kawaida la sadaka iliyotolewa kwa bwana kwa kuteketezwa kwa moto.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nayo itakuwa ya Haruni na wanawe; nao wataila katika mahali patakatifu; kwa sababu kwake ni takatifu sana katika sadaka zitolewazo kwa BWANA kwa moto, kwa amri ya milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aroni na wazawa wake peke yao ndio wanaoruhusiwa kula mikate hiyo kwani ni mitakatifu kabisa kwa sababu ni sehemu ya sadaka ninazotolewa mimi Mwenyezi-Mungu kwa moto. Hiyo ni haki yao milele.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha hiyo mikate itakuwa yao Haroni na wanawe, nao sharti waile mahali patakatifu. Kwa kuwa mitakatifu yenyewe sharti iwe fungu lao litokalo kwenye mioto ya Bwana. Hii na iwe haki yao ya kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nayo itakuwa ya Haruni na wanawe; nao wataila katika mahali patakatifu; kwa sababu kwake ni takatifu sana katika sadaka zisongezwazo kwa BWANA kwa moto, kwa amri ya milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haruni na wazao wake peke yao ndio wanaoruhusiwa kula mikate hiyo maana ni mitakatifu kabisa kwa sababu ni sehemu ya sadaka ninazotolewa mimi Yawe kwa moto. Hiyo ni haki yao milele.