Leviticus 25:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwaka wa hamsini mtauheshimu kwa kutangaza uhuru kwa watumwa wote nchini. Mwaka huo utakuwa ni sikukuu ya ukumbusho wa miaka hamsini. Kila mmoja wenu atairudia mali yake na jamaa yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwaka wa hamsini mtauweka wakfu na kutangaza uhuru katika nchi kwa wakazi wake wote. Itakuwa ni Yubile kwenu; kila mmoja wenu atairudia mali ya jamaa yake, na kila mmoja kurudi kwenye ukoo wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwaka wa hamsini mtauheshimu kwa kutangaza uhuru kwa watumwa wote nchini. Mwaka huo utakuwa ni sikukuu ya ukumbusho wa miaka hamsini. Kila mmoja wenu atairudia mali yake na jamaa yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwaka wa hamsini mtauweka wakfu na kutangaza uhuru katika nchi kwa wakazi wake wote. Itakuwa ni yubile kwenu; kila mmoja wenu atairudia mali ya jamaa yake, na kila mmoja kurudi kwenye ukoo wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwaka wa hamsini mtauweka wakfu na kutangaza uhuru katika nchi kwa wakazi wake wote. Itakuwa ni yubile kwenu; kila mmoja wenu atairudia mali ya jamaa yake, na kila mmoja kurudi kwenye ukoo wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kuwatangazia uhuru watu wote katika nchi; itakuwa ni mwaka wa jubilii kwenu; na kila mtu atairudia milki yake, na kila mtu atarejea kwa jamaa yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwaka wa hamsini mtauheshimu kwa kutangaza uhuru kwa watumwa wote nchini. Mwaka huo utakuwa ni sikukuu ya ukumbusho wa miaka hamsini. Kila mmoja wenu atairudia mali yake na jamaa yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwaka huo wa 50 sharti mwutakase na kuwatangazia wote wakaao katika nchi yenu, ya kuwa wamekwisha kukombolewa. Mwaka huo uwe wa kupiga shangwe kwenu, mkirudia kila mtu mali zilizokuwa zake, tena mkirudi kila mtu kwa ndugu zake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote wanayokaa; itakuwa ni yubile kwenu; nanyi kila mtu atairudia milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwaka wa makumi tano mutauheshimu kwa kutangaza uhuru kwa watumwa wote katika inchi. Mwaka huo utakuwa ni sikukuu ya ukumbusho wa miaka makumi tano. Kila mumoja wenu atarudilia mali yake na jamaa yake.