Leviticus 25:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa kuwa mwaka huo, ni wa sikukuu ya ukumbusho wa miaka hamsini, msipande mbegu au kuvuna chochote kiotacho chenyewe wala kuchuma zabibu kutoka miti msiyoipogoa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwaka wa hamsini utakuwa Yubile kwenu, msipande wala msivune kile kinachoota chenyewe, au kuvuna zabibu zisizohudumiwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa kuwa mwaka huo, ni wa sikukuu ya ukumbusho wa miaka hamsini, msipande mbegu au kuvuna chochote kiotacho chenyewe wala kuchuma zabibu kutoka miti msiyoipogoa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwaka wa hamsini utakuwa yubile kwenu, msipande wala msivune kile kiotacho chenyewe, au kuvuna zabibu zisizohudumiwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwaka wa hamsini utakuwa yubile kwenu, msipande wala msivune kile kiotacho chenyewe, au kuvuna zabibu zisizohudumiwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni jubilii kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizichume zabibu za mizabibu isiyopelewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa kuwa mwaka huo, ni wa sikukuu ya ukumbusho wa miaka hamsini, msipande mbegu au kuvuna chochote kiotacho chenyewe wala kuchuma zabibu kutoka miti msiyoipogoa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli mwaka huo wa hamsini sharti uwe kwenu mwaka wa kupiga shangwe, msipande mbegu, wala msiyavune yatakayoota yenyewe, wala msiyachume mazao ya mizabibu, msiyoitunza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu mwaka huo ni wa sikukuu ya ukumbusho wa miaka makumi tano, musipande mbegu au kuvuna chochote kinachoota chenyewe wala kuchuma zabibu kutoka miti musiyokata matawi.