Leviticus 25:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bei ya ardhi ni lazima ilingane na miaka kabla ya kurudishwa kwa mwenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utanunua ardhi kwa mzawa wa nchi yako kulingana na hesabu ya miaka baada ya Yubile. Naye muuzaji ataiuza kwako kulingana na hesabu ya miaka iliyobaki ya kuvuna mavuno.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya yubile, ndivyo utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bei ya ardhi ni lazima ilingane na miaka kabla ya kurudishwa kwa mwenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Utanunua ardhi kwa mzawa wa nchi yako kwa misingi ya hesabu ya miaka baada ya Yubile. Naye ataiuza kwako kwa misingi ya hesabu ya miaka iliyobaki kwa kuvuna mavuno.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Utanunua ardhi kwa mzawa wa nchi yako kwa misingi ya hesabu ya miaka baada ya Yubile. Naye ataiuza kwako kwa misingi ya hesabu ya miaka iliyobaki kwa kuvuna mavuno.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya jubilii, ndivyo utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bei ya ardhi ni lazima ilingane na miaka kabla ya kurudishwa kwa mwenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukinunua shamba kwa mwenzako, sharti mwihesabu miaka iliyopita tangu mwaka wa shangwe, ndipo akuuzie kwa kuipunguza hiyo miaka, aliyolivuna.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya yubile, ndivyo utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bei ya shamba inapaswa kulingana na miaka mbele ya kurudishwa kwa mwenyeji.