Leviticus 25:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Waambie Waisraeli hivi: Mtakapofika katika nchi ninayowapeni mimi Mwenyezi-Mungu kila mwaka wa saba nchi itapumzishwa isilimwe kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi ninayowapa ninyi, nchi yenyewe ni lazima ishike sabato kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika nchi niwapayo, ndipo hiyo nchi itashika Sabato kwa ajili ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Waambie Waisraeli hivi: Mtakapofika katika nchi ninayowapeni mimi Mwenyezi-Mungu kila mwaka wa saba nchi itapumzishwa isilimwe kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi ninayowapa ninyi, nchi yenyewe ni lazima ishike Sabato kwa ajili ya BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi ninayowapa ninyi, nchi yenyewe ni lazima ishike Sabato kwa ajili ya bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika nchi niwapayo, ndipo hiyo nchi itashika Sabato kwa ajili ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Waambie Waisraeli hivi: Mtakapofika katika nchi ninayowapeni mimi Mwenyezi-Mungu kila mwaka wa saba nchi itapumzishwa isilimwe kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sema na wana wa Isiraeli na kuwaambia: Mtakapoingia katika nchi hiyo, nitakayowapa, hiyo nchi nayo sharti ipate kumpumzikia Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapoingia katika nchi niwapayo, ndipo hiyo nchi itashika Sabato kwa ajili ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uwaambie Waisraeli hivi: Mutakapofika katika inchi ninayowapa mimi Yawe, kila mwaka wa saba inchi itapumzishwa isilimwe kwa heshima ya Yawe.