Leviticus 25:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama nyumba iliyo katika mji uliojengewa ukuta haikukombolewa kwa muda wa mwaka mmoja, basi, itakuwa mali ya yule aliyeinunua milele katika vizazi vyao vyote; wala haitarudishwa katika mwaka wa sikukuu ya kukumbuka miaka hamsini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa haikukombolewa kabla ya mwaka mmoja kamili kupita, nyumba iliyo ndani ya mji uliozungukwa kwa ukuta itakuwa mali ya kudumu ya mnunuzi na wazao wake. Haitarudishwa Mwaka wa Yubile.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama haikukombolewa katika muda wa mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyo ndani ya mji wenye kuta itathibitishwa milele kuwa ya huyo aliyeinunua, katika vizazi vyake; nayo haitatoka katika yubile.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama nyumba iliyo katika mji uliojengewa ukuta haikukombolewa kwa muda wa mwaka mmoja, basi, itakuwa mali ya yule aliyeinunua milele katika vizazi vyao vyote; wala haitarudishwa katika mwaka wa sikukuu ya kukumbuka miaka hamsini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa haikukombolewa kabla ya mwaka mmoja kamili kupita, nyumba iliyo ndani ya mji uliozungukwa kwa ukuta itakuwa mali ya kudumu ya mnunuzi na wazao wake. Haitarudishwa mwaka wa Yubile.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa haikukombolewa kabla ya mwaka mmoja kamili kupita, nyumba iliyo ndani ya mji uliozungukwa kwa ukuta itakuwa mali ya kudumu ya mnunuzi na wazao wake. Haitarudishwa mwaka wa Yubile.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kama haikukombolewa katika muda wa mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyo ndani ya mji wenye kuta itathibitishwa milele kuwa ya huyo aliyeinunua, katika vizazi vyake; nayo haitatoka katika jubilii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama nyumba iliyo katika mji uliojengewa ukuta haikukombolewa kwa muda wa mwaka mmoja, basi, itakuwa mali ya yule aliyeinunua milele katika vizazi vyao vyote; wala haitarudishwa katika mwaka wa sikukuu ya kukumbuka miaka hamsini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini isipokombolewa, hata mwaka wote mzima utimie, basi, hiyo nyumba iliyomo mjini mwenye boma itakuwa kabisa kabisa yake aliyeinunua kuwa yake yeye mwenyewe na ya vizazi vyake, haitatoka kwao katika mwaka wa shangwe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama haikukombolewa katika muda wa mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyo ndani ya mji wenye kuta itathibitishwa milele kuwa ya huyo aliyeinunua, katika vizazi vyake; nayo haitatoka katika yubile.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama nyumba inayokuwa katika muji uliojengewa ukuta haikukombolewa kwa muda wa mwaka mumoja, basi, itakuwa mali ya yule aliyeinunua milele katika vizazi vyao vyote, wala haitarudishwa katika mwaka wa sikukuu ya kukumbuka miaka makumi tano.