Leviticus 25:33 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ikiwa mmoja wa Walawi haitumii haki yake ya kukomboa, basi, nyumba iliyouzwa ni lazima irudishwe kwa mwenyewe katika mwaka wa kukumbuka miaka hamsini, kwani nyumba zilizomo katika miji wanayomiliki Walawi wamepewa kama sehemu yao kutoka kwa watu wa Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo mali ya Mlawi inaweza kukombolewa, yaani nyumba iliyouzwa katika mji wowote wanaoushikilia itarudishwa Mwaka wa Yubile, kwa sababu nyumba zilizo katika miji ya Walawi ni mali yao miongoni mwa Waisraeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena kama mtu mmoja wa hao Walawi akikomboa, ndipo nyumba iliyouzwa, na mji wa milki yake, itatoka katika yubile; maana, hizo nyumba za miji ya Walawi ni milki yao kati ya wana wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ikiwa mmoja wa Walawi haitumii haki yake ya kukomboa, basi, nyumba iliyouzwa ni lazima irudishwe kwa mwenyewe katika mwaka wa kukumbuka miaka hamsini, kwani nyumba zilizomo katika miji wanayomiliki Walawi wamepewa kama sehemu yao kutoka kwa watu wa Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo mali ya Mlawi inaweza kukombolewa, yaani nyumba iliyouzwa katika mji wo wote wanaoushikilia itarudishwa mwaka wa Yubile, kwa sababu nyumba zilizo katika miji ya Walawi ni mali yao miongoni mwa Waisraeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo mali ya Mlawi inaweza kukombolewa, yaani nyumba iliyouzwa katika mji wowote wanaoushikilia itarudishwa mwaka wa Yubile, kwa sababu nyumba zilizo katika miji ya Walawi ni mali yao miongoni mwa Waisraeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mtu mmoja wa hao Walawi akikomboa nyumba iliyouzwa na mji wa milki yake, itatoka katika jubilii; maana, hizo nyumba za miji ya Walawi ni milki yao kati ya wana wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ikiwa mmoja wa Walawi haitumii haki yake ya kukomboa, basi, nyumba iliyouzwa ni lazima irudishwe kwa mwenyewe katika mwaka wa kukumbuka miaka hamsini, kwani nyumba zilizomo katika miji wanayomiliki Walawi wamepewa kama sehemu yao kutoka kwa watu wa Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama mtu anakomboa kwao Walawi nyumba au mji, katika mwaka wa shangwe itatoka kwake na kukoma kuwa mali yake, kwani nyumba za miji ya Walawi ni fungu lao walilopewa kuwa lao kabisa katikati ya wana wa Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena kama mtu mmoja wa hao Walawi akikomboa, ndipo nyumba iliyouzwa, na mji wa milki yake, itatoka katika yubile; maana, hizo nyumba za miji ya Walawi ni milki yao kati ya wana wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikiwa mumoja wa Walawi hatumii haki yake ya kukomboa, basi, nyumba iliyouzishwa ni lazima irudishwe kwa mwenyeji katika mwaka wa kukumbuka miaka makuni tano, maana nyumba zinazokuwa katika miji Walawi wanayorizi wamepewa kama sehemu yao kutoka kwa watu wa Israeli.