Leviticus 25:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mwaka wa saba utakuwa ni sabato ya mapumziko rasmi; ni sabato ya Mwenyezi-Mungu. Msipande chochote wala kuipogoa mizabibu yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini katika mwaka wa saba, nchi lazima iwe na sabato ya mapumziko, sabato kwa Mwenyezi Mungu. Msipande mbegu katika mashamba yenu, wala msikate mizabibu yenu matawi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini katika mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi, ni Sabato kwa Bwana; usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mwaka wa saba utakuwa ni sabato ya mapumziko rasmi; ni sabato ya Mwenyezi-Mungu. Msipande chochote wala kuipogoa mizabibu yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mwaka wa saba nchi lazima iwe na Sabato ya mapumziko, ni Sabato kwa BWANA. Msipande mbegu katika mashamba yenu, wala msikate mizabibu yenu matawi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mwaka wa saba nchi lazima iwe na Sabato ya mapumziko, Sabato kwa bwana. Msipande mbegu katika mashamba yenu, wala msikate mizabibu yenu matawi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini katika mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi, ni Sabato kwa BWANA; usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mwaka wa saba utakuwa ni sabato ya mapumziko rasmi; ni sabato ya Mwenyezi-Mungu. Msipande chochote wala kuipogoa mizabibu yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mwaka wa saba sharti uiwie nchi yako mwaka wa kupumzika kabisa, nayo ipate kumpumzikia Bwana. Hapo usipande mbegu mashambani kwako, wala usiikatie mizabibu yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini katika mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi, ni Sabato kwa BWANA; usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mwaka wa saba utakuwa ni Sabato ya mapumziko, ni Sabato ya Yawe. Musipande chochote wala kukata matawi ya mizabibu yenu.