Leviticus 25:46 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hao watumwa unaweza kuwakabidhi kwa watoto wako wawe mali yao milele. Hao unaweza kuwafanya watumwa wako, lakini kuhusu ndugu yako Mwisraeli, usimtawale kwa ukatili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Unaweza kuwafanya hao kuwa urithi wa watoto wako, na unaweza kuwafanya watumwa kwa maisha yao yote. Lakini usiwatawale ndugu zako Waisraeli kwa ukatili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi mtawafanya kuwa urithi kwa watoto wenu baada yenu, wawe milki yao; siku zote mtatwaa watumwa wenu katika hao; lakini msitawale kwa nguvu juu ya ndugu zenu, hao wana wa Israeli, wenyewe kwa wenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hao watumwa unaweza kuwakabidhi kwa watoto wako wawe mali yao milele. Hao unaweza kuwafanya watumwa wako, lakini kuhusu ndugu yako Mwisraeli, usimtawale kwa ukatili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hao waweza kuwarithisha watoto wako kuwa urithi wao na wanaweza kuwafanya watumwa maisha yao yote, lakini usiwatawale ndugu zako Waisraeli kwa ukatili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hao waweza kuwarithisha watoto wako kuwa urithi wao, na wanaweza kuwafanya watumwa maisha yao yote, lakini usiwatawale ndugu zako Waisraeli kwa ukatili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi mtawafanya kuwa urithi kwa watoto wenu baada yenu, wawe milki yao; siku zote mtatwaa watumishi wenu kwa hao; lakini msitawale kwa nguvu juu ya ndugu zenu, hao wana wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hao watumwa unaweza kuwakabidhi kwa watoto wako wawe mali yao milele. Hao unaweza kuwafanya watumwa wako, lakini kuhusu ndugu yako Mwisraeli, usimtawale kwa ukatili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata wana wenu wataokuwa nyuma yenu mtaweza kuwaachilia hao kuwa urithi wao wa mali zitakazokuwa zao kale na kale, nao mwafanyishe kazi za utumwa. Lakini ndugu zenu walio wana wa Isiraeli msitawalane wenyewe na wenyewe kwa ukorofi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi mtawafanya kuwa urithi kwa watoto wenu baada yenu, wawe milki yao; siku zote mtatwaa watumwa wenu katika hao; lakini msitawale kwa nguvu juu ya ndugu zenu, hao wana wa Israeli, wenyewe kwa wenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hao watumwa unaweza kuwapatia watoto wako wakuwe mali yao milele. Hao unaweza kuwafanya watumwa wako, lakini kuelekea ndugu yako Mwisraeli, usimutawale kwa kinguvu.