Leviticus 25:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Chochote kinachoota peke yake msikivune wala kuchuma zabibu kutoka miti isiyopogolewa. Huo utakuwa mwaka wa kuipumzisha ardhi rasmi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msivune chochote kinachoota chenyewe, wala kuvuna zabibu zenu ambazo hamkuzihudumia. Nchi lazima iwe na mwaka wa mapumziko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hicho kimeacho chenyewe katika mavuno yako, usikivune, wala zabibu za mizabibu isiyopelewa usizitunde; utakuwa mwaka wa kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Chochote kinachoota peke yake msikivune wala kuchuma zabibu kutoka miti isiyopogolewa. Huo utakuwa mwaka wa kuipumzisha ardhi rasmi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msivune na kuweka akiba kinachoota chenyewe, wala kuvuna na kusindika zabibu ambayo hamkuhudumia mashamba yake. Nchi lazima iwe na mwaka wa mapumziko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Msivune na kuweka akiba kinachoota chenyewe, wala kuvuna na kusindika zabibu ambayo hamkuhudumia mashamba yake. Nchi lazima iwe na mwaka wa mapumziko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hicho kimeacho chenyewe katika mavuno yako, usikivune, wala zabibu za mizabibu isiyopelewa usizichume; utakuwa mwaka wa kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Chochote kinachoota peke yake msikivune wala kuchuma zabibu kutoka miti isiyopogolewa. Huo utakuwa mwaka wa kuipumzisha ardhi rasmi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo masazo ya mavuno yako, kama yataota yenyewe, usiyavune, wala zabibu zitakazozaliwa na mizabibu, usiyoitunza, usizichume, kwani mwaka huu sharti uwe kabisa mwaka wa mapumziko ya nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hicho kimeacho chenyewe katika mavuno yako, usikivune, wala zabibu za mizabibu isiyopelewa usizitunde; utakuwa mwaka wa kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Chochote kinachoota peke yake musikivune wala kuchuma zabibu kutoka miti isiyokatwa matawi. Huo utakuwa mwaka wa kupumzisha udongo.