Leviticus 25:52 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama miaka michache imepungua kabla ya kufikia sikukuu ya ukumbusho wa miaka hamsini, atahesabu kiasi cha bei iliyobaki kulingana na miaka hiyo na kumlipa hiyo fidia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa miaka iliyobaki ni michache kufikia Mwaka wa Yubile, atafanya hesabu yake, naye atalipa malipo yanayostahili kwa ajili ya ukombozi wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena kwamba imesalia miaka michache tu hata mwaka wa yubile, ndipo atafanya hesabu naye, kama hesabu ya miaka yake ilivyo, ndivyo atakavyolipa tena bei ya ukombozi wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama miaka michache imepungua kabla ya kufikia sikukuu ya ukumbusho wa miaka hamsini, atahesabu kiasi cha bei iliyobaki kulingana na miaka hiyo na kumlipa hiyo fidia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa miaka iliyobaki ni michache kufikia Mwaka wa Yubile, atafanya hesabu yake naye atalipa malipo yanayostahili kwa ajili ya ukombozi wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa miaka iliyobaki ni michache kufikia Mwaka wa Yubile, atafanya hesabu yake, naye atalipa malipo yanayostahili kwa ajili ya ukombozi wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena kama imesalia miaka michache tu hadi mwaka wa jubilii, ndipo atafanya hesabu naye, kama hesabu ya miaka yake ilivyo, ndivyo atakavyolipa tena bei ya ukombozi wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama miaka michache imepungua kabla ya kufikia sikukuu ya ukumbusho wa miaka hamsini, atahesabu kiasi cha bei iliyobaki kulingana na miaka hiyo na kumlipa hiyo fidia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kama miaka iko michache bado, mpaka mwaka wa shangwe utakapotimia, basi, na azirudishe hizo tu ziipasazo hiyo miaka yake michache kuwa makombozi yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena kwamba imesalia miaka michache tu hata mwaka wa yubile, ndipo atafanya hesabu naye, kama hesabu ya miaka yake ilivyo, ndivyo atakavyolipa tena bei ya ukombozi wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama miaka michache imepunguka mbele ya kufikia kwa sikukuu ya ukumbusho wa miaka makumi tano, atahesabu sehemu ya bei iliyobaki kulingana na miaka hiyo na kumulipa hayo malipo.