Leviticus 26:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Msijitengenezee sanamu za miungu ya uongo, msishike sanamu zao za kuchonga wala nguzo wala sanamu za mawe yaliyochongwa nchini mwenu na kuvisujudu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Msijitengenezee sanamu, au kusimamisha sanamu ya kuchonga, au jiwe la kuabudia, na pia msijiwekee jiwe lililochongwa katika nchi yenu ili kulisujudia. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Msifanye sanamu yo yote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jiwe lo lote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Msijitengenezee sanamu za miungu ya uongo, msishike sanamu zao za kuchonga wala nguzo wala sanamu za mawe yaliyochongwa nchini mwenu na kuvisujudu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Msijitengenezee sanamu au kusimamisha kinyago cha kuchonga, mnara, wala jiwe la kuabudia, pia msijiwekee jiwe lililochongwa katika nchi yenu na kusujudu mbele yake. Mimi ndimi BWANA Mungu wenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Msijitengenezee sanamu au kusimamisha kinyago cha kuchonga, au mnara, wala jiwe la kuabudia, na pia msijiwekee jiwe lililochongwa katika nchi yenu na kusujudu mbele yake. Mimi ndimi bwana Mwenyezi Mungu wenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Msifanye sanamu yoyote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jiwe lolote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Msijitengenezee sanamu za miungu ya uongo, msishike sanamu zao za kuchonga wala nguzo wala sanamu za mawe yaliyochongwa nchini mwenu na kuvisujudu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Msijitengenezee vinyago vilivyo vya bure! Wala msijisimamishie mifano ya Mungu iliyochongwa kwa miti wala ya nguzo zilizoyeyushwa kwa shaba, wala msijipatie katika nchi yenu mawe yenye machorochoro ya kuyaangukia. Kwani mimi Bwana ni Mungu wenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Msifanye sanamu yo yote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jiwe lo lote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musijitengenezee sanamu za miungu ya uongo, musishike sanamu zao za kuchongwa wala nguzo wala sanamu za mawe yaliyochongwa katika inchi yenu na kuviabudu. Mimi ni Yawe, Mungu wenu.