Leviticus 26:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, niliyewatoa nchini Misri ili msiwe watumwa wa Wamisri. Mimi nimevunja nira mliyofungiwa shingoni mwenu na kuwafanya mtembee wima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili msiendelee kuwa watumwa wa Wamisri, nikavunja nira yenu, na kuwawezesha kutembea mkiwa mmeinua vichwa vyenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, niliyewaleta mtoke katika nchi ya Misri, ili msiwe watumwa wao; nami nimeivunja miti ya kongwa lenu, nikawaendesha mwende sawasawa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, niliyewatoa nchini Misri ili msiwe watumwa wa Wamisri. Mimi nimevunja nira mliyofungiwa shingoni mwenu na kuwafanya mtembee wima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi ndimi BWANA Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili msiendelee kuwa watumwa wa Wamisri, nikavunja kongwa lenu na kuwawezesha kutembea mkiwa mmeinua vichwa vyenu juu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi ndimi bwana Mwenyezi Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili msiendelee kuwa watumwa wa Wamisri, nikavunja kongwa lenu, na kuwawezesha kutembea mkiwa mmeinua vichwa vyenu juu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewaleta mtoke katika nchi ya Misri, ili msiwe watumwa wao; nami nimeivunja miti ya kongwa lenu, nikawafanya mwende sawasawa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, niliyewatoa nchini Misri ili msiwe watumwa wa Wamisri. Mimi nimevunja nira mliyofungiwa shingoni mwenu na kuwafanya mtembee wima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi Bwana ni Mungu wenu aliyewatoa katika nchi ya Misri, msiwe watumwa wao, nayo miti ya makongwa yenu nikaivunja, nikawapa kujiendea na kujinyosha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewaleta mtoke katika nchi ya Misri, ili msiwe watumwa wao; nami nimeivunja miti ya kongwa lenu, nikawaendesha mwende sawasawa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi ni Yawe, Mungu wenu, niliyewatoa katika inchi ya Misri kusudi musikuwe watumwa wa Wamisri. Mimi nimevunja nira muliyofungiwa katika shingo lenu na kuwafanya mutembee wima.