Leviticus 26:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi nitawakabili, nanyi mtapigwa na adui zenu; mtatawaliwa na wale wanaowachukia. Mtatishwa na kukimbia hata kama hakuna mtu yeyote anayewafukuza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitauelekeza uso wangu dhidi yenu ili mshindwe na adui zenu; wale wanaowachukia watawatawala, nanyi mtakimbia ingawa hakuna mtu anayewafukuza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitauelekeza uso wangu kinyume chenu, nanyi mtapigwa mbele ya adui zenu; hao wawachukiao watatawala juu yenu; nanyi mtakimbia wakati ambao hapana awafukuzaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi nitawakabili, nanyi mtapigwa na adui zenu; mtatawaliwa na wale wanaowachukia. Mtatishwa na kukimbia hata kama hakuna mtu yeyote anayewafukuza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitauelekeza uso wangu dhidi yenu ili kwamba mshindwe na adui zenu; wale wanaowachukia watawatawala, nanyi mtakimbia ingawa hakuna mtu anayewafukuza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitauelekeza uso wangu dhidi yenu ili mshindwe na adui zenu; wale wanaowachukia watawatawala, nanyi mtakimbia ingawa hakuna mtu anayewafukuza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitauelekeza uso wangu kinyume chenu, nanyi mtapigwa mbele ya adui zenu; hao wawachukiao watatawala juu yenu; nanyi mtakimbia wakati ambao hapana awafukuzaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi nitawakabili, nanyi mtapigwa na adui zenu; mtatawaliwa na wale wanaowachukia. Mtatishwa na kukimbia hata kama hakuna mtu yeyote anayewafukuza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao uso wangu nitaugeuza, uwapingie, mpigwe mbele ya adui zenu, nao wachukivu wenu wawatwale; nanyi mtajikimbilia pasipo kuona aliyewakimbiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitauelekeza uso wangu kinyume chenu, nanyi mtapigwa mbele ya adui zenu; hao wawachukiao watatawala juu yenu; nanyi mtakimbia wakati ambao hapana awafukuzaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi nitawashambulia, nanyi mutapigwa na waadui zenu. Mutatawaliwa na wale wanaowachukia. Mutatishwa na kukimbia hata kama hakuna mutu yeyote anayewafukuza.