Leviticus 26:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitawapeleka wanyama wakali kati yenu ambao watawanyakulieni watoto wenu na kula mifugo yenu; na kukata idadi yenu hata njia zenu zigeuke kama jangwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawatuma wanyama mwitu dhidi yenu, nao watawaibieni watoto wenu, watawaangamiza ng’ombe wenu, na kuifanya idadi yenu kuwa ndogo, hivi kwamba barabara zenu zitakuwa hazina watu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitaleta wanyama wakali kati yenu, ambao watawanyang'anya watoto wenu, na kuwaharibu wanyama wenu wa kufugwa, na kuwapunguza muwe wachache hesabu yenu; na njia zenu zitakuwa ni ukiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitawapeleka wanyama wakali kati yenu ambao watawanyakulieni watoto wenu na kula mifugo yenu; na kukata idadi yenu hata njia zenu zigeuke kama jangwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawatuma wanyama mwitu dhidi yenu, nao watawaibieni watoto wenu, watawaangamiza ng'ombe wenu na kuifanya idadi yenu kuwa ndogo hivi kwamba barabara zenu zitakuwa hazina watu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawatuma wanyama mwitu dhidi yenu, nao watawaibieni watoto wenu, watawaangamiza ng’ombe wenu, na kuifanya idadi yenu kuwa ndogo, hivi kwamba barabara zenu zitakuwa hazina watu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitaleta wanyama wakali kati yenu, ambao watawanyang'anya watoto wenu, na kuwaharibu wanyama wenu wa kufugwa, na kuwapunguza hesabu yenu; na njia zenu zitakuwa ni ukiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitawapeleka wanyama wakali kati yenu ambao watawanyakulieni watoto wenu na kula mifugo yenu; na kukata idadi yenu hata njia zenu zigeuke kama jangwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitatuma kwenu nyama wa porini, wawaue watoto wenu, wawatoweshe nao nyama wenu wa kufuga, nanyi wenyewe watawapunguza, mwe wachache, nazo njia za kwenu ziwe pasipo watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitaleta wanyama wakali kati yenu, ambao watawanyang’anya watoto wenu, na kuwaharibu wanyama wenu wa kufugwa, na kuwapunguza muwe wachache hesabu yenu; na njia zenu zitakuwa ni ukiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitaleta nyama wakali kati yenu ambao watawanyanganya watoto wenu na kula mifugo yenu na kupunguza hesabu yenu hata njia zenu zigeuke kama jangwa.