Leviticus 26:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitawaleteeni upanga ambao utalipiza kisasi juu ya agano mlilovunja. Nyinyi mtakimbilia katika miji yenu, lakini nitawapelekea maradhi mabaya na kuwatia mikononi mwa adui zenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitawaletea upanga juu yenu ili kuwapatiliza kwa kuvunja agano langu. Mtakapokimbilia mijini mwenu, nitatuma tauni kati yenu, nanyi mtatiwa mikononi mwa adui zenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitaleta upanga juu yenu, utakaopatiliza kisasi cha hilo agano; nanyi mtakutanishwa ndani ya miji yenu; nami nitaleta tauni kati yenu; nanyi mtatiwa mkononi mwa adui.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitawaleteeni upanga ambao utalipiza kisasi juu ya agano mlilovunja. Nyinyi mtakimbilia katika miji yenu, lakini nitawapelekea maradhi mabaya na kuwatia mikononi mwa adui zenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawaletea upanga juu yenu ili kuwapatiliza kwa kuvunja Agano langu. Mtakapokimbilia mijini mwenu, nitatuma tauni katikati yenu, nanyi mtatiwa mikononi mwa adui zenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawaletea upanga juu yenu ili kuwapatiliza kwa kuvunja Agano langu. Mtakapokimbilia mijini mwenu, nitatuma tauni katikati yenu, nanyi mtatiwa mikononi mwa adui zenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitaleta upanga juu yenu, utakaopatiliza kisasi cha hilo agano; nanyi mtakutanishwa ndani ya miji yenu; nami nitaleta tauni kati yenu; nanyi mtatiwa mikononi mwa adui.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitawaleteeni upanga ambao utalipiza kisasi juu ya agano mlilovunja. Nyinyi mtakimbilia katika miji yenu, lakini nitawapelekea maradhi mabaya na kuwatia mikononi mwa adui zenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nitapeleka kwenu upanga utakaowalipiza kisasi kwa kulivunja Agano; tena mtakapokusanyika mijini mwenu nitatuma kwenu ugonjwa uuao upesi, kisha mtatiwa mikononi mwa adui zenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitaleta upanga juu yenu, utakaopatiliza kisasi cha hilo agano; nanyi mtakutanishwa ndani ya miji yenu; nami nitaleta tauni kati yenu; nanyi mtatiwa mkononi mwa adui.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawaletea upanga ambao utalipiza kisasi juu ya agano mulilovunja. Ninyi mutakimbilia katika miji yenu, lakini nitawaletea ugonjwa mukali na kuwatia katika mikono ya waadui zenu.