Leviticus 26:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitapaharibu mahali penu pa ibada milimani, nitazibomoa madhabahu zenu za kufukizia ubani, na kuzitupa maiti zenu juu ya sanamu za miungu yenu. Roho yangu itawachukia kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitaharibu mahali penu pa juu pa kuabudia, nibomoe madhabahu yenu ya kufukizia uvumba, na kuzilundika maiti zenu juu ya sanamu zenu zisizo na uhai, nami nitawachukia ninyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, na kuziangusha sanamu zenu za jua, nami nitaitupa mizoga yenu juu ya mizoga ya sanamu zenu; na roho yangu itawachukia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitapaharibu mahali penu pa ibada milimani, nitazibomoa madhabahu zenu za kufukizia ubani, na kuzitupa maiti zenu juu ya sanamu za miungu yenu. Roho yangu itawachukia kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitapaharibu mahali penu pa juu pa kuabudia miungu, nitabomoa madhabahu zenu za kufukizia uvumba na kuzilundika maiti zenu juu ya sanamu zenu zisizo na uhai, nami nitawachukia ninyi sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitapaharibu mahali penu pa juu pa kuabudia miungu, nibomoe madhabahu zenu za kufukizia uvumba, na kuzilundika maiti zenu juu ya sanamu zenu zisizo na uhai, nami nitawachukia ninyi sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, na kuziangusha sanamu zenu za jua, nami nitaitupa mizoga yenu juu ya mizoga ya sanamu zenu; na roho yangu itawachukia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitapaharibu mahali penu pa ibada milimani, nitazibomoa madhabahu zenu za kufukizia ubani, na kuzitupa maiti zenu juu ya sanamu za miungu yenu. Roho yangu itawachukia kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Napo penu pa kutambikia vilimani nitapabomoa, nayo mifano yenu ya jua nitaitowesha, nayo mizoga yenu nitaitupa juu ya vipande vya magogo yenu ya kutambikia, kwani Roho yangu itakuwa imechukizwa nanyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, na kuziangusha sanamu zenu za jua, nami nitaitupa mizoga yenu juu ya mizoga ya sanamu zenu; na roho yangu itawachukia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitaharibu pahali penu pa ibada kule juu ya milima, nitabomoa mazabahu zenu za kufukizia ubani, na kutupa maiti zenu juu ya sanamu za miungu yenu. Roho yangu itawachukia kabisa.