Leviticus 26:36 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na kwa baadhi yenu watakaosalimika nitawaletea woga mioyoni mwao, katika nchi ya adui zao hata jani linalopeperushwa litawakimbiza. Watakimbia kama mtu anayekimbia vita. Watakimbia na kuanguka hata kama hamna mtu anayewafukuza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Kwa habari ya wenzenu wale watakaobaki, nitaifanya mioyo yao kuwa na hofu kuu katika nchi za adui zao, kiasi kwamba sauti ya jani linalopeperushwa na upepo itawafanya wakimbie. Watakimbia kana kwamba wanakimbia upanga, nao wataanguka, ijapokuwa hakuna anayewafukuza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena hao wa kwenu watakaobaki, nitawatilia woga mioyoni mwao, katika hizo nchi za adui zao; na sauti ya jani lililopeperushwa itawakimbiza; nao watakimbia, kama mtu akimbiavyo upanga; nao wataanguka hapo ambapo hapana afukuzaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na kwa baadhi yenu watakaosalimika nitawaletea woga mioyoni mwao, katika nchi ya adui zao hata jani linalopeperushwa litawakimbiza. Watakimbia kama mtu anayekimbia vita. Watakimbia na kuanguka hata kama hamna mtu anayewafukuza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Kwa habari ya wenzenu wale watakaobaki, nitaifanya mioyo yao kuwa na hofu kuu katika nchi za adui zao kiasi kwamba sauti ya jani linalopeperushwa na upepo itawafanya wakimbie. Watakimbia kana kwamba wanakimbia upanga, nao wataanguka, ingawa hakuna anayewafukuza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Kwa habari ya wenzenu wale watakaobaki, nitaifanya mioyo yao kuwa na hofu kuu katika nchi za adui zao, kiasi kwamba sauti ya jani linalopeperushwa na upepo itawafanya wakimbie. Watakimbia kana kwamba wanakimbia upanga, nao wataanguka, ingawa hakuna anayewafukuza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena hao wa kwenu watakaobaki, nitawatia woga mioyoni mwao, katika hizo nchi za adui zao; na sauti ya jani lililopeperushwa itawakimbiza; nao watakimbia, kama mtu akimbiavyo upanga; nao wataanguka hapo ambapo hapana afukuzaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na kwa baadhi yenu watakaosalimika nitawaletea woga mioyoni mwao, katika nchi ya adui zao hata jani linalopeperushwa litawakimbiza. Watakimbia kama mtu anayekimbia vita. Watakimbia na kuanguka hata kama hamna mtu anayewafukuza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao watakaosalia kwenu nitawalegeza mioyo yao, wakikaa katika nchi ya adui zao, shindo la jani kavu linalopeperushwa na upepo liwakimbize, wakimbie, kama watu wanavyokimbizwa na upanga, waanguke, pasipo kuona aliyewakimbiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena hao wa kwenu watakaobaki, nitawatilia woga mioyoni mwao, katika hizo nchi za adui zao; na sauti ya jani lililopeperushwa itawakimbiza; nao watakimbia, kama mtu akimbiavyo upanga; nao wataanguka hapo ambapo hapana afukuzaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kwa njia ya wamoja wenu watakaobaki nitaleta woga ndani ya moyo wao, katika inchi ya waadui zao hata jani linalopeperushwa litawakimbiza. Watakimbia kama mutu anayekimbia vita. Watakimbia na kuanguka hata kama hakuna mutu anayewafukuza.