Leviticus 26:43 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wakati watakapokuwa nje ya nchi yao, nchi hiyo itafurahia sabato zake hapo itakapokuwa hali ya ukiwa. Wakati huo wao watatubu uovu wao wa kupuuza maagizo yangu na kuyachukia maagizo yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa wataiacha nchi ukiwa, nayo itafurahia sabato zake wakati itakuwa ukiwa bila wao. Wataadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao, kwa sababu walizikataa sheria zangu na kuzichukia amri zangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nchi nayo itaachwa na wao, nayo itazifurahia Sabato zake, itakapokuwa ukiwa pasipokuwa na wao; nao wataikubali adhabu ya uovu wao; kwa sababu, naam, ni kwa sababu wamezikataa hukumu zangu, na roho zao zimezichukia amri zangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wakati watakapokuwa nje ya nchi yao, nchi hiyo itafurahia sabato zake hapo itakapokuwa hali ya ukiwa. Wakati huo wao watatubu uovu wao wa kupuuza maagizo yangu na kuyachukia maagizo yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa wataiacha nchi ukiwa, nayo itafurahia Sabato zake wakati ikiwa ukiwa pasipo wao kuwepo. Watalipizwa kwa ajili ya dhambi zao, kwa sababu walizikataa sheria zangu na kuzichukia amri zangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa wataiacha nchi ukiwa, nayo itafurahia Sabato zake wakati itakuwa ukiwa bila wao. Wataadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao, kwa sababu walizikataa sheria zangu na kuzichukia amri zangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nchi nayo itaachwa na wao, nayo itazifurahia Sabato zake, itakapokuwa ukiwa pasipokuwa na wao; nao wataikubali adhabu ya uovu wao; kwa sababu wameyakataa maagizo yangu, na roho zao zimezichukia amri zangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wakati watakapokuwa nje ya nchi yao, nchi hiyo itafurahia sabato zake hapo itakapokuwa hali ya ukiwa. Wakati huo wao watatubu uovu wao wa kupuuza maagizo yangu na kuyachukia maagizo yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kwanza sharti nchi itokwe nao, ipate kuifurahia miaka yake ya mapumziko ikiwa pori tupu kwa kuachwa nao; nao kwanza sharti waitikie, ya kuwa walikora manza walipoyatupa maamuzi yangu, roho zao zikayachukia maongozi yangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nchi nayo itaachwa na wao, nayo itazifurahia Sabato zake, itakapokuwa ukiwa pasipokuwa na wao; nao wataikubali adhabu ya uovu wao; kwa sababu, naam, ni kwa sababu wamezikataa hukumu zangu, na roho zao zimezichukia amri zangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati watakapokuwa inje ya inchi yao, inchi hiyo itafurahia Sabato zake hapo itakapokuwa katika hali ya ukiwa. Wakati huo wao watatubu uovu wao wa kuzarau maagizo yangu na kuchukia masharti yangu.